UA-45153891-1

Monday, February 17, 2014

TUZO ZA MUZIKI ZA KILIMANJARO TANZANIA (KTMA) 2014 ZAZINDULIWA LEO, MABORESHO YAONGEZWA



Tuzo za  muziki za Kilimanjaro mwaka 2014 zimezinduliwa leo  February 17, 2014 na  mabadiliko kadhaa yakiwa yamefanyika.Tuzo hizo ambazo hutolewa kwa wasanii wa muziki mbalimbali wa Tanzania zilianzishwa mwaka 1999.

George Kavishe kutoka TBL ambao ndio wadhamini wa tuzo hizi amesema maboresho makubwa ambayo yamefanyika mwaka huu ni tofauti na mara zote ambazo wamekua wakihusisha watanzania dakika za kupiga kura tu na hivyo kukosa nafasi ya kupendekeza nani aingie kwenye kipengele 'category' gani. "Mwaka huu tumebadilisha kutokana na matakwa ya soko hivyo Watanzania ndio watapendekeza nani aingizwe kwenye category gani. Kupitia Magazeti, website ya Kilimanjaro na vipeperushi kuanzia kesho February 18 2014 kutaonyeshwa category zote za mwaka huu za kupigiwa kura na wananchi na watanzania watatuma kura zao kupitia simu za mkononi kupitia 15440, ambapo kila mmoja atapendekeza msanii, kikundi au producer gani aingie kwenye kipengele flani", alisema Kavishe.
Aliendelea kusema kwamba  mwaka huu watanzania watapiga kura mara mbili ambapo ya kwanza ni nani aingie kwenye category alafu baadae tena kupiga kura nani awe mshindi wa kwanza, yaani mwaka huu ile timu ya watu 100 ya waandishi, watangazaji na wadau wa muziki kuchagua nani na nani aingie kwenye category haitofanya hivyo bali itakutana kuhakikisha tu kama wimbo uliopendekezwa na wananchi ni wa mwaka husika, uko sehemu husika na pia kama umekidhi vigezo vya kuingia.

Mabadiliko ya tuzo za mwaka huu wa 2014 kwa mujibu wa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) ni kwamba, ni kutokana na maoni na mapendekezo ya wadau wa tasnia ya muziki kutoa sababu mbalimbali.
Mwaka huu KTMA itakua na category 36 ambapo category 34 ni za kuchaguliwa na mbili zilizobaki ni zile maalum za kuteuliwa.

Mwaka 2013 kulikua na category 37 ambapo Mwaka huu imeondolewa moja kutokana na maoni mbalimbali ya wadau wa muziki ambapo category yenyewe ni Mtayarishaji chipukizi wa mwaka.

Category zilizobadilishwa majina mwaka huu 2014 ni Mtumbuizaji bora wa kike wa muziki badala ya msanii bora wa kike ilivyokua mwaka jana, mtumbuizaji bora wa kiume wa muziki badala ya msanii bora wa kiume mwaka jana, mwimbaji bora wa kiume Taarab ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume Taarab.

Mwimbaji bora wa kiume bongofleva badala ya mwaka jana Msanii bora wa kiume bongofleva, mwimbaji bora kiume  'band' ambayo mwaka jana ilikua msanii bora wa kiume band, mwimbaji bora wa kike Bongofleva badala ya mwaka jana msanii bora wa kike Bongofleva.

Mwimbaji bora wa kike Taarab badala ya mwaka jana msanii bora wa kike Taarab, mwimbaji bora wa kike band badala ya msanii bora wa kike band.

Basata wanasema neno 'MSANII' halitatumika kwa sababu neno hilo linasadifu au linaleta maana za kuingia zaidi ya kitu kimoja, kunaweza kuwepo na msanii wa uchongaji, msanii wa uchoraji n.k,  kwa kuwa wote  wanafanya kazi ya sanaa. Hivyo  watatumia majina ya kimuziki kwa sababu huku ni kwenye muziki.

Pia mwaka huu kutakua na video bora ya muziki ya mwaka badala ya video bora ya wimbo kwa kuwa neno muziki lina uwanja mpana kuliko wimbo. Kutakua na wimbo bora wa Afropop badala ya wimbo bora wa bongopop, kutakua na wimbo bora wenye vionjo vya asili ya kitanzania badala ya wimbo bora wenye vionjo vya asili.

Zaidi ya hapo, kutakuwa na nsanii bora chipukizi anaeibukia badala ya msanii bora anaechipukia, maana wapo wasanii wengi sana chipukizi huko mitaani na muziki wao haujasikika, inawezekana wamekaa miaka mingi wakifanya kazi zao lakini wakaibuka na kuonekana.

No comments:

Post a Comment