Siku kadhaa zilizopita kupitia vyombo mbalimbali vya habari kumekuwa na taarifa kuhusu kufungiwa kwa video ya 'Nimevurugwa' ya Snura. Bado haijajulikana wazi kama aliyefungiwa ni Snura au video yake, maana kwa mujibu wa kaimu katibu mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) chombo kinachohusika na kufungia video moja kwa moja ni bodi ya filamu Tanzania.
Sakata hilo linafuatia wasiwasi wa kimaadili juu ya video hiyo ya Snura
ambaye inasemekana amehamua kutoa video ya kukonga nyoyo za mashabiki
wake ambao baada ya video iliyopita ya wimbo wa 'Majanga' aliambiwa na
mashabiki wake kwamba amewaangusha kwani hawakutegemea itoke vile. Hivyo
yote haya yanatokea baada ya kuwapa mashabiki wake kile wakitakacho.
Basata wanahusika na Audio ambapo kama imekiuka maadili msanii anaambiwa arekebishe, pia wanazingatia ubunifu wa msanii kabla kazi haijaingia sokoni kwa kufuatia suala la urasimishaji. "‘Suala la kufungiwa kwa Snura najua kabisa linaenda kwenye suala la maadili na limeandikwa sana na sisi Baraza kama Baraza tunaangalia sana suala la maadili tukisema tunamfungia hatufungii video tu tunamfungia msanii mwenyewe". Alinukuliwa na mtandao wa millardayo.com kaimu katibu mtendaji wa Basata Bw.Godfrey Mungeleza.
No comments:
Post a Comment