UA-45153891-1

Thursday, February 13, 2014

PHARRELL WILLIAMS NA LUPITA NYONG'O WAKIWA KWENYE UZINDUZI WA TUZO ZA ACADEMMY 2014


Mtayarishaji machachali wa muziki, muimbaji na mwandishi wa nyimbo wa nchini Marekani Pharrell Williams ameonekana akiwa karibu sana na muigizaji wa kike wa Hollywood ambaye ni mkenya Lupita Nyong’o.  Pharrell  mwenye umri wa miaka 40 japo anaonekana mdogo, alishindwa kuondoka bila kupiga picha na mwanadada huyo walipokutana katika hoteli ya Beverly Hilton Hotel jimboni California, siku ya Jumatatu Februari 10, 2014  kwenye uzinduzi wa tuzo za Academy za mwaka 2014 ambapo wote wametajwa kwenye vipengela vya  wanaowania tuzo hizo ambazo ni za 86.
Pharrell yuko katika kipengele cha ‘Wimbo bora’ ambao ni “Happy” na Lupita  yuko kipengele cha ‘Muigizaji bora anayezipa nguvu kazi zake’. Watu wataanza kuwapigia kura washiriki wa tuzo hizo February 14  mpaka February 25, 2014 na tuzo zitatolewa rasmi kwa washindi Machi 2, 2014.

No comments:

Post a Comment