UA-45153891-1

Saturday, November 10, 2012

MSHINDI WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 NI WALTER CHILAMBO


 
Hawa ndio washiriki watano waliokuwa wamebakia
kutoka katika mchujo tangu ebss 2012 ilipoanza safari yake.
Kutoka kushoto ni  Nsami Nkwabi, Walter Chilambo, Salma Yusuph, Wababa Mtuka na Nshoma Ng'hangasamala            


FAINALI YENYEWE

Kushoto ni washiriki watatu ambao waliingia kumi bora na kulia ni baadhi ya washiriki watatu  ambao walifika hatua ya tano bora.Wakiwa pamoja, ni baada ya kuburudisha kwa wimbo wa pamoja muda mfupi kabla ya fainali ya shindano hilo
Washiriki watano bora wakiwa tayari kuanza kazi, wenye suti ni washereheshaji wa tukio hilo lililofanyika ndani ya ukumbi Diamond Jubilee
 Nsami Nkwabi ndiye aliyefungua dimba akisindikizwa na Barnaba.
 Kila mmoja kwanza alipanda jukwaani na mwanamuziki maarufu kwa kuimba wimbo wa mwanamuziki huyo. Hapa ni Nshoma Ng'hangasamala  akitamba na miondoko ya mwambao wa Pwani.
Salma Yusuph na Linex 
 Wababa na Mwasiti
 Walter na Ditto
 Baada ya Kolabo kila mmoja alisimama kama yeye.Huyu si mwingine bali Nsami Nkwabi !
Baada ya Nsami alifuata Nshoma.Hawa wawili ni mtu na dada yake.
 Salma!!!!!  Msichana mwenye kipaji cha  pekee
 
 Wengine wanamuita "Wafather", wengine "Wadad", huyu si mwingine ni Wababa akiokota mshiko baada ya kuwapa raha mashabiki wake.



Walter  Chilambo  akifanya mambo
 MC’s kijana mtanashati Caesar Daniel na mwana dada mrembo Vanessa Mdee ndio wanasongesha show nzima ya Epiq Bongo Star Search
Majaji wa Epiq Bongo Star Search wakiwa kazini! 
Mashabiki wa Walter wakifanya vitu vyao!
 Na mashabiki wa Wababa kama kawaida!
 Mshindi wa BSS 2010 akitoa burudani
Show ilisindikizwa na burudani toka kwa wasanii  mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya
THT Dancers
  Ommy Dimpoz 


 Linah na Amin
 Mzee Yusuph
 Washiriki watatu waliendelea kubaki kati ya hawa
 Salma Yusuph
 Wababa Mtuka
 Walter Chilambo 
 
 Wote wanaweza lakini mshindi lazima apatikane.Mmoja wao aliishia hapa kimashindano
Aimbapo utatamani kumtunza lakini waweza shindwa kutokana na sauti yake nzuri na hisia zitakavyokugandisha kwenye kiti ulichokalia 
 Bila kujali mwanamuziki ni wa jinsia gani,inasemekana shabiki namba moja wa mwanamuziki ni mwanamke, alafu mwanaume anafuata. Wanawake wanashangilia, wanatunza, wanapiga kura. Pamoja na uwezo na sauti nzuri aliyonayo Walter Chilambo,unazani  pia alifanikiwa katika hilo?.Pia nakumbuka maneno ya jaji Master J aliposema,"Walter pamoja na sauti yako nzuri una bahati sketi zinakuzimia, kila la kheri".
 Haya sasa!
Chief Judge wa EBSS Bi. Lita Paursen maarufu kama Madam Lita, akitoa maelezo mafupi kabla ya kumpa CCO wa Zantel nafasi amtangaze mshindi 
CCO wa Zantel ambao ndio wadhamini wa shindano hilo akisubiri kuondoa kiu ya matazamaji. 
Walter Chilambo baada ya kutangazwa mshindi wa EBSS 2012 
Madam Lita akimpoza Salma nakumpongeza kwa hatua nzuri aliyofikia 
 Walter akikabidhiwa zawadi yake ya milion 50Tsh
 Walter akiondoka baada ya kufanya yake

No comments:

Post a Comment