UA-45153891-1

Monday, April 29, 2013

OMMY DIMPOZ ATAREKODI WIMBO NA KUNDI LA R2BEES LA NCHINI GHANA?


BAADA ya kutangazwa kwa wasanii wa muziki walioingia kwenye kinyang’anyiro cha tuzo za muziki wa Tanzania yaani “Kilimanjaro Tanzania Music Awards” Aprili 25 mwaka huu, mwanamuziki Farji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’ anaonekana kwenye vipengere 7 vya tuzo hizo. Hiyo ni baada ya takribani siku 5 tangu zilipotangazwa tuzo za muziki wa nchini Ghana zijulikanazo kama Vodafone Ghana Muzic Awards ambazo zimezinduliwa Aprili 20  mwaka huu.

Katika tuzo hizo za nchini Ghana, kundi la muziki lenye wanamuziki wawili Paedae na Mugeez, linalojulikana kama R2Bees ndilo  lililoongoza kwa kutajwa  mara nyingi zaidi kwenye vipengere vya tuzo hizo. Jina la kundi hilo limetokea kwenye vipengere 8 ikiwa ni pamoja na kipengere cha wimbo bora wa mwaka, kipengere ambacho Ommy Dimpoz pia ameingia kwa tuzo za muziki za hapa nchini Tanzania. Pia mmoja  wa wanamuziki wa kundi hilo anayeitwa Mugeez ameingia kwenye vipengere vya msanii bora wa kiume na mtunzi bora wa mashairi, sawa na Ommy Dimpoz kwenye msanii bora wa kiume kwa ujumla na mtunzi bora wa mashairi wa Bongo Flava.  

Ommy Dimpoz ni miongoni mwa wanamuziki wa nchini Tanzania wanaofanya vizuri na tayari ameanza kujitangaza kimataifa kwa kurekodi nyimbo za kushirikiana na wanamuziki mbalimbali barani Afrika akiwemo J.Martin wa Nigeria. 

Kama mdau wa muziki na msimamizi wa Blog ya Datsongwritertz, namshauri Ommy Dimpoz  kurekodi wimbo na kundi hilo la nchini Ghana. Katika tuzo za muziki za mwaka huu nchini Ghana, R2Bees wanashindanisha wimbo wao wa Life (Walahi) na nyimbo za wakali wengine kama Azonto Fiesta wa Appietus, Sarkodie na Kesse, Antenna wa Fuse ODG na nyimbo zingine kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka. Katika kipengere hicho kwa tuzo za muziki za Tanzania, Ommy Dimpoz anashindanisha wimbo wa Me n U aliomshirikisha mwanadada Vanessa Mdee na nyimbo zingine kali ambazo ni Dear God ya Kala Jeremiah, Leka Dutigite ya Kigoma all stars, Mapito ya Mwasiti akimshirikisha Ally Nipishe na Pete ya Ben Pol.

Ommy Dimpoz

 Kushoto ni Paedae na kulia ni Mugeez wa R2Bees

No comments:

Post a Comment