TAFSIRI ya neno Diamond kwa
kiswahili ni Almasi ambayo ni moja ya madini yenye thamani kubwa. Bila shaka mwanamuziki Nasibu Abdul “Diamond
Platnumz” analitendea haki jina hilo, nalo pia linamtendea haki. Msanii huyo wa
Bongo Flava mwenye uwezo mkubwa jukwaani ni miongoni mwa wanamuziki wenye mashabiki
wengi Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla. Mbali na jina hilo, pia
anafahamika kama rais wa Wasafi na sukari ya warembo.
Katika pitapita za mitaani,
imegundulika kwamba jina lake pia limezaa majina mengine mawili ambayo ni Dai-mond
na Dia-mond. Ni majina ambayo yanasikika kutoka kwa baadhi ya mashabiki wake
wanaoshindwa kulitamka jina lake vile inavyotakiwa.
Diamond ambaye kwa sasa yuko
nchini Uingereza, mwaka huu yuko kwenye tuzo za muziki wa Tanzania “Kilimanjaro
Tanzania Music Awards” kwenye vipengere vya msanii bora wa kiume kwa ujumla na
msanii bora wa kiume Bongo Flava.
Diamond akiwa kazini
No comments:
Post a Comment