UA-45153891-1

Thursday, May 30, 2013

MWANA FA, AAHIRISHA SHOW YAKE YA "THE FINEST" KWA HESHIMA YA NGWAIR.


Kwa heshima ya Ngwea, Mwana FA ametangaza kuahirisha show yake y The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013. 

Kutokana na habari za kufariki kwa mwanamuziki Albert Mangwair, msanii ambaye ni mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Mwanamuziki mwingine pia wa Hip Hop Hamis Mwin'jumah, a.k.a MwanaFA(Pichani)nametangaza kuahirisha show yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013.


Mwana FA ameelezea kwenye mtandao wa kijamii "Twitter" kuguswa kwake na taarifa hizi kumesababisha ajisikie kuomboleza kwanza, kabla maisha mengine hayajaendelea, kwa hiyo amewaomba radhi mashabiki, hasa wale waliokuwa wameshanunua tiketi, na kuwaomba wawe na subira, tarehe ya show itratangazwa tena baada ya mwili wa marehemu kuletwa na kupumzishwa.

HABARI; www.jestina-george.com 

No comments:

Post a Comment