UA-45153891-1

Saturday, May 11, 2013

SNURA NA SHILOLE MAJANGA



MWANAMUZIKI na muigizaji wa kike Snura Mushi 'Snura', ametumia zaidi ya dakika 45 kuzungumza na mashabiki wake juu ya ugomvi wake na Zuwena Mohamed 'Shilole' ambaye pia ni mwanamuziki na muigizaji. Mwanadada huyo anayetamba na wimbo wa “Majanga” ambao kwa sasa ndiyo habari ya mjini kwenye vituo mbalimbali vya redio na mitaani, alisema Shilole amekuwa akimtuhumu kuwa kaiga staili yake ya uimbaji.

Snura kupitia Amplifier ya Clouds FM juzi, alisikika akisema staili yake ya uimbaji ni tofauti kabisa na ile ya Shilole. Alifafanua kwamba Shilole anaimba staili ya mduara wakati yeye hafanyi muziki wa aina hiyo ingawa hakuweka bayana aina ya muziki anayoifanya yeye. Aliendelea kusema kwamba Watanzania wanaweza kuwafananisha yeye na Shilole kama waigizaji wa kike ambao pia ni wanamuziki, lakini sio kwa aina ya muziki waufanyao. Pia alisisitiza kuwa, tofauti ya aina zao za muziki ni kama Marekani na Chanika.





No comments:

Post a Comment