UA-45153891-1

Thursday, May 30, 2013

ALICHOKIANDIKA LADY JAYDEE KUHUSU KUAHIRISHA SHOO YAKE YA MIAKA 13 BAADA YA KIFO CHA NGWAIR

 
Judith Wambura 'Lady Jaydee'.

Ifuatayo ni taarifa aliyoitoa msanii Judith Wambura 'Lady Jaydee' katika ukurasa wake wa Facebook kuhusu kuahirisha shoo yake iliyokuwa ifanyike kesho katika ukumbi wa Nyumbani Lounge jijini Dar...
Tunaomba radhi kwa watu wote ambao mlikuwa mmeshanunua tickets za miaka 13 ya Lady Jaydee ambapo onyesho ilikuwa lifanyike Ijumaa ya tar 31 Mei 2013.
Tunapenda kuwataarifu kuwa onyesho hilo limesitishwa kutokana na msiba mzito wa msanii mwenzetu Ngwair mpaka hapo tutakapo wataarifu tena.
Tunasubiri taratibu za kuupokea mwili na tarehe ya maziko, baada ya hapo tutaendelea na ratiba za show na tutawatangazia tarehe inayofuata ambayo si mbali baada ya maziko.
Wale mliokwisha nunua tickets naomba mzitunze tickets zenu, kwani ndio hizo hizo mtakazozitumia siku ya show hata kama tarehe imebadilishwa.
Natanguliza shukrani na naomba radhi kwa usumbufu wowote nitakaokuwa nimewasababishia.
Kila kitu kitaendelea kama kilivyokuwa kimepangwa, hapo baadae.


HABARI KUTOKA www.globalpublishers.info

No comments:

Post a Comment