Majaji wa Shindano la The Vodacom Mic King, kutoka kushoto ni John Dilinga Mathlou (JD), Abdallah Mrisho (Abby Cool) wa Global Publishers na Producer Ally Baucha wa Baucha Records.
Pembeni mwa majaji, kushoto ni msanii wa Hip Hop, Stamina na kulia ni Producer Tudd Thomas, nyuma ni washiriki wa shindano hilo.
Waandishi
wa habari na wageni wengine
Washiriki wa shindano la The Vodacom Mic King na gari atakalopewa mshindi
MSHINDI wa kwanza, wa pili na wa tatu wa shindano la The Vodacom Mic King linaloandaliwa na uongozi wa Dar Live chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya producer mahiri nchini Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Atriums Mei 21, 2013, meneja matukio wa Dar Live Bw. Abdallah Mrisho amesema, jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi wa kwanza ataondoka na gari aina ya TOYOTA FUNCARGO (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Tamasha la shindano hili litafanyika Mei 25, 2013 katika uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem au kwa jina linguine Mbagala Rangi Tatu.
Majaji katika shindano hilo ni DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou (JD), Producer Ally Baucha kutoka Baucha Records na mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho au Abby Cool wa Kampuni ya Global Publishers. Shindano hili ni la muziki wa Kurap au Hip Hop ambalo lina lengo la kuwaendeleza vijana wenye lengo la kufanya muziki katika maisha yao.

Stamina, Tudd Thomas na mmoja wa waandishi wa habari baada ya mkutano.
Tudd Thomas, John Dilinga (JD), Stamina na Ally Baucha
Dat (Mwandishi wa nyimbo,
matangazo na Blogger wa datsongwritertz Blog) akiwa na Tudd Thomas muda mfupi baada ya mkutano na waandishi wa habari
No comments:
Post a Comment