UA-45153891-1

Sunday, June 26, 2016

UCHAMBUZI- JINSI YA KUPATA AINA YA MUZIKI INAYOWAKILISHA TANZANIA

Ndugu wasomaji wa  gazeti tanzu hili la semadat, niwaombe radhi kwa kusitisha habari  na makala zangu kwa kipindi cha nyuma kisichopungua mwaka mmoja. Ilikuwa ni katika arakati  zangu za kuendelea kuunganisha vipaji na ujuzi  kama ilivyo kauli mbiu ya maisha yangu yaani “Combining my talents and Skills”. Sasa tunaendelea na leo tunaanza kwa ni jinsi gani inaweza kupatikana aina ya  muziki unaowakilisha nchi ya Tanzania.

Siku moja  niliulizwa na mdau mmoja wa muziki  kwamba “Unauonaje muziki wa Tanzania”, Nikamwambia “Muziki wa Tanzania unakua, unazaa na hivyo unahitaji nafasi au mazingira mazuri ya kulea na kukuza. Linaweza lisiwe jibu lililozoeleka katika masikio ya walio wengi maana katika hili wengi huzungumzia mafanikio ya yanayoonekana kwa mwanamuziki mmojammoja, hamasa kubwa ya wadau vikiwemo vyombo vya habari, makampuni na Taasisi mbalimbali zinavyowekeza katika sanaa hii na kuufanya muziki kuwa biashara na jinsi jamii inavyoupokea na kuukubali tofauti na siku za nyuma. Hii ni sawa kabisa, ni miongoni mwa viashiria vya ukuaji wa sanaa hii.

Lakini tukiuzungumzia muziki wenyewe kiashiria kikubwa  cha ukuaji wake ni jinsi ambavyo unaanza kujitegemea. Katika baadhi ya nchi kama Afrika kusini na Nigeria, sio kwamba hakuna aina zingine za muziki nchini humo kama nchi ya Tanzania ilivyo na Muziki wa Dansi, Mchiriku au Mnanda, Taarabu na zingine nyingi zikiwemo za asili kama ile ya Saida Karoli. Kilichotokea katika nchi hizo ni kwamba, zilijitokeza aina zingine za muziki ambazo ziliakisi muziki wa Amerika na Ulaya kwa muda lakini baadae zikarudi nyumbani kwao. Hapo ndipo ikapatikana Kwaito ya Africa Kusini na ile inayoitwa Niger Style ya Nigeria.
Nimetumia nchi hizo mbili kama kiwakilishi kwa nchi zingine za Afrika ambazo zimefikia hatua hiyo na kwa kuwa huo ndio muziki wa kizazi kipya wa nchi hizo sasa nirudi katika muziki wa kizazi kipya wa Tanzania yaani “Bongo Flava”.

Ninapozungumzia muziki wa Tanzania kwa sasa nazungumzia muziki huu wa kizazi kipya  lakini kwa kuhusisha aina zilizokuwepo kabla ya Bongo Flava, ambazo baadhi nimezitaja ndipo narejea katika  mambo matatu ambayo ni kukua, kuzaa na kukuza.

Katika maisha ya kawaida kifamilia, mtoto anapokuwa mkubwa anaondoka nyumbani, lakini kimuziki mtoto anapokuwa mkubwa anarudi nyumbani.
Ikumbukwe kwamba Muziki huu wa kizazi kipya, ulianza kwa kuakisi aina mbili za muziki wa Marekani ambazo ni Hip-Hop na RnB. Lakini leo muziki huu umerudi Afrika, ndiyo maana vionjo vinavyotawala katika muziki huu ni Afro beat, Afro Pop, Zouk, Rumba, Chacha na zingine nyingi za hapa hapa Afrika. Hiyo ni hatua ya kwanza katika kukua kwa muziki huu.
Hatua inayofuata ni muziki huu kurudi hapahapa nchini Tanzania kwa maana ya kuakisi muziki uliyokuwepo awali. Hiyo imeshaanza kutokea. Tunashuhudia msanii maarufu kama Diamond Platnumz akiunganisha muziki wake na mitindo ya Taarabu (Mduara), Mnanda na nyinginezo. Sikiliza pia kwa makini vionjo vya muziki anaofanya AY kwa sasa. Wapo pia ambao wameanza kuuchanganya na midundo, melodia na lugha za asili kuufanya muziki huu kuwa wa kitanzania zaidi.

Kwa Muziki huu  kurudi nchini Tanzania, zinajitokeza aina flani za muziki ambazo  siyo Bongo Flava ya miaka ya 1990-2000. Hao ndio watoto wanaozaliwa ambao wanatakiwa kulelewa. Watoto hao ndiyo watatupa aina ya  Muziki itakayotutambulisha. Kadiri watoto hao wanavyozidi kuwa wengi kila mmoja atakuwa akileta hamasa kwa mwingine na  tabia zao kufanana na hatimaye kufanya kitu kimoja. Hiyo ndiyo itakuwa hatua ya ukomavu.

Kuna mijadala na maswali kwamba aina ya muziki inayoitambulisha Tanzania ni ipi, kwa kuwa hata “Bongo Flava” siyo aina  ya muziki, bali jina linalowakilisha aina mbali mbali za muziki wa kizazi kipya. Kweli itaendelea kuwa hivi. Inaweza kuchukua hata zaidi ya muhongo mmoja kuanzia sasa, lakini kwa kupitia hatua hizo ambazo zimeshaanza kujitokeza itakapofika  hatua hiyo ya ukomavu ndipo kitapatika kile kinachofahamika kama ‘Identity’ ya muziki wa Tanzania.

4 comments:

  1. Oh my God! It is too creepy for my mind! This girl wanted to attract attention, but eventually the public was shocked. Help me to forget her face, please! https://tuko.co.ke/152818-woman-grown-huge-beard-attract-date-guys-online.htmlо

    ReplyDelete
  2. Just look! That's great! Interesting blog. I read the best news. I recently read about the sexual problems of the family, how to properly be able to teach it to children, and more. If anyone is interested, read here https://tuko.co.ke/192789-kenyan-men-share-embarassing-moments.html

    ReplyDelete
  3. Thanks for the great article writing; well structured. You make assimilation easy and you have great contents.
    See helpful:
    Unskilled $1000/5hr Paying Jobs in UK
    Casual high Paying jobs in Australia

    ReplyDelete