UA-45153891-1

Wednesday, April 2, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AZUNGUMZIA KAMPENI YA KILIMO YA ONE.ORG INAYOITWA'Do Agric'


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz ambaye ni miongoni mwa wanamuziki 19 wa Afrika waliochaguliwa kukutana  nchini Nigeria ili kushiriki katika wimbo wa pamoja wa kuhamasisha vijana kujiunga na kilimo, amesikika akizungumzia kampeni hiyo leo kupitia Clouds FM. 

"Kilimo si ushamba, tajiri wa kwanza Afrika Aliko Dangote ni mkulima pia. Unaweza kuwa na shughuri zako mjini lakini ukawa mkulima pia kupitia watu uliowaajiri ambao wanafanya kazi moja kwa moja shambani, inawezekana pia kwa watu kama sisi ambao wengine wanatuita wauza sura", alisema Diamond ambaye pia akiwa jijini Lagos, amefanikiwa kumalizia wimbo wake anaofanya na staa wa nchini humo 'Iyanya' ambaye alikuwa hapa nchini Tanzania mwaka jana katika msimu wa Fiesta.


Wasanii wengine wanaoshiriki katika kampeni hiyo ya 'Do Agric, It pays' ambayo ni kifupi kwa Kiingereza, yaani "Do Agriculture, it pays" ni pamoja na D’Banj na Femi Kuti wa Nigeria,  Fally Ipupa wa DR Congo,  Tiken Jah Fakoly wa Cote d’Ivoire,  Juliani wa Kenya na  Judith Sephuma wa Afrika Kusini.

Maelezo zaidi kuhusu Kampeni hiyo iliyozinduliwa March 31, 2014 yanapatikana katika mtandao wa www.one.org, na humo pia unaweza kuupata wimbo wa pamoja wa wasanii hao.

No comments:

Post a Comment