UA-45153891-1

Wednesday, April 2, 2014

MR NICE BADILI MATUKIO HASI KUWA CHANYA



Sina uhakika kama uko facebook, twitter, Insatagram au kwingine niweze hata kushauri chochote kupitia akaunti yako. Labda tu niseme kupitia semadat, sina shaka waweza pata ujumbe huu kupitia watu wengine ambao uko karibu nao na wako mtandaoni. Kaka  umaarufu wako ni mkubwa sana. Mpaka mwanzoni mwa mwaka jana, wewe na  Saida Kalori ndiyo wasanii pekee wa muziki wa Tanzania mliokuwa mkitolewa mifano mpaka na viongozi wataalam wa masoko katika mada mbalimbali za nembo au alama  mashuhuri za watu kwa kuzungumzia mtu mmoja mmoja au kwa lugha ya Kiingereza wanasema 'Personal Branding'.


Hebu sasa tuzungumzie matukio yako ya ugomvi yanayojirudia ambayo yanapelekea kupigwa na kuumizwa ambayo ni mara ya nne sasa!. Vyanzo vya matukio vinafanana ambapo vinahusisha wanawake, chanzo ikiwa ni wewe kaka ambaye kwa mfano hili la mwishoni mwa Machi 2014, limetokana na wewe kumfuata mwanamke ambaye mwenza wake akufurahishwa na kitendo hicho na kufuatia kipigo kikali kwako. Tazama jinsi unavyotazamwa na jamii.Vyombo vya habari ikiwemo mitandao maarufu wala hawaandiki kwa kufurahi kwa sababu wamepata habari! La hasha!, ni kuwafahamisha watu ili pia watoto wadogo uliokuwa ukiimba nao "Kidali Po" wafahamu kwamba sivyo msanii anavyotakiwa kuishi.

Tuachane na hiyo ishu 'brother'. Sasa si unajua katika maisha kuna kuteleza lakini si kuanguka?. Weka mikakati jipange ndugu. Pengine ni kwa sababu una muda mwingi sana wa kukaa 'Bar'. Mbona kipindi kile cha enzi za "Kuku kapanda Baiskeli" haikuwa hivi?. Ulikuwa bize na 'show' uongo kweli?. Kama muziki kwasasa umekataa fanya mambo mengine kwa kutumia jina lako. Hivi unafahamu kwamba kama ungelinda heshima yako au kile kitu waingereza wanasema 'Personality', kampuni yoyote ingeweza kutengeneza na kuuza bidhaa kwa jina lako huku wewe ukilamba noti kupitia mkataba mnono?. Hilo ni moja tu, yapo mengi sana. Niulize swali pia, hivi tangu uanze muziki mpaka leo hujagundua kipaji chako kingine?. Kwa mfano imethibitika kwamba wanamuziki wengi wanaweza kufanya fani zingine mbalimbali za sanaa vizuri pia.

Ndugu tukiachana na vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya hapa nchini. Umeandikwa sana nchi zingine hasa Afrika Mashariki ikiwa pamoja na mtandao unaoitwa Ghafra wa nchini Kenya. Wazo langu ni kwamba wewe bado ni 'Icon' kwenye sekta ya burudani, hebu kwa wazo la haraka wafuate hata wataalam wa masuala ya uandishi wa vitabu vya hadithi wakuandikie 'series' ya matukio hayo, alafu waitoe ibadilishwe kuwa filamu. Ndugu yangu kuwa 'flexible' siyo tu kubadili staili katika fani husika, bali pamoja na kucheki fani zingine. Wewe unafurahi tu kuona ukipita sehemu watu wanataja jina lako?. Sasa tumia hilo jina kutengeneza pesa badala ya kutengeneza damu. Inawezekana, mastaa wengi wanatengeneza pesa kupitia matukio mbalimbali yaliyowai kuwakuta. Badili matukio hasi kuwa chanya. For the love of creativity.


1 comment: