Kala Jeremiah baada ya kufanya vizuri katika ngoma yake inayokwenda kwa jina la Dear God, aliweka wazi kwamba siku ya tarehe 20 mwezi huu anatarajia kutoka na
album yake mpya inayokwenda kwa jina la Pasaka.Na hapo juu anaonyesha
cover yake mpya ya hiyo album.
.
Thursday, December 13, 2012
Monday, December 10, 2012
RAY C AMEPONA: LEO AMEPATA NAFASI YA KUMTEMBELEA RAIS JAKAYA KIKWETE IKULU JIJINI DAR
Mwanamuziki wa Bongo Fleva maarufu kama Ray C siku ya leo amemtembelea Rais Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam na kumshukuru kwa msaada wa matibabu kipindi alipokuwa mgonjwa.
Kwa upande wa mama mzazi wa Ray C amemshukuru sana Raisi Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye.
Kwa upande wa mama mzazi wa Ray C amemshukuru sana Raisi Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Ray C kushoto ni Mama yake mzazi Ray C Bibi Margareth Mtweve na kulia ni Sarah Mtwere Dada yake Ray C.
Habari kutoka Dj fetty blog
Habari kutoka Dj fetty blog
Thursday, December 6, 2012
ALICHOKIANDIKA NONINI KUHUSU PRODUZA P FUNK MAJANI NA PICHA YA MAJANI AMBAYO NONINI AMEIWEKA KWENYE WALL YAKE
Hiyo ni picha ambayo msanii kutoka Kenya Nonini ambaye pia ni mtangazaji
alitupia kwenye Wall yake asubuhi,akaambatanisha na ujumbe huuu:
"Producer na mmiliki wa Bongo Records,
P.Funk 'Majani',Hakuna msani wa Bongo hajafanya kazi na P- funk pande
ya hip hop….Kutoka Kina Proffesor,FidQ,Ngwea na Jaymoe Kimya
Kimya....(Huyu ni Daktari Musyoka Wao)"
Monday, December 3, 2012
FID Q AMTAMBULISHA DOGO ALIYEMFUNDA KWA MIEZI 9
Mwanamuziki
mkongwe wa Hip hop Fid Q , almaarufu kama Ngosha the Don, amesema
ameamua kumchukua mwanafunzi mmoja na kumfundisha Muziki ili
mwanafunzi huyo aweze kupambana na ushindani mkubwa uliopo kutoka kwa
wasanii mbali mbali kwenye Muziki.
Akiongea kupitia kituo kimoja cha Radio leo jijini Dar-Es-Salaam, Fid
Q alisema anaona fahari kuwa msanii anayetoa fursa kwa vijana badala ya
wao (vijana) kumtegemea kwa kolabo ama pesa lakini kwa kuwafunda yeye
mwenyewe wataweza kujihudumia wenyewe katika siku za baadae.
Fid Q amekuwa mfano mzuri sana wa kuigwa katika ubunifu na moyo wa
kujitolea, na katika siku za hivi karibuni kupitia mahojiano
tuliyoyafanya naye msanii Stamina, alionyesha kumkubali sana Fid Q, na
kusema ni mtu anayemtegemgea kwenye Muziki wa Hip Hop kwa sababu
anamuona kama ni nguzo na msingi wa Hip Hop hapa bongo.
Stamina alisema “kama kuna msanii ambaye ninamkubali sana, basi ni
Fid Q , kwani ni msanii pekee aliyesoma vitabu vingi sana ndiyo maana
haishiwi mashairi, pamoja na uwezo wake wa kuchana.
Aidha Fid Q alisema mwanzoni aliwawachukua vijana 6 ambao bado walikuwa
hawajakomaa, kwa hiyo akawafanya kama wanafunzi na kuwafundisha muziki,
na hatimae sasa mmoja wao amemaliza masomo na kuwa msanii ambaye
aliyeiva kimuziki.
Fid Q alisema “nimeamua kuwafundisha vijana muziki ili wawe na uwezo
kama wangu na kuwapa fursa katika maisha yao kwa sababu ni vigumu
sana mtu kumpa kazi ambayo itamsaidia kimaisha ila ukimpa fursa
utamsaidia sana kuliko kumpa pesa. Alimalizia.
A.Y ASHEREKEA PARTY YAKE NA WATU MBALIMBALI BAADA YA KUPATA TUZO YA CHANNEL "O"
Msanii wa Bongo Fleva almaarufu kama A.Y.baada ya kuwania tuzo ya Channel O Most Gifted East African Award huko nchini South African.
Siku ya jana katika maeneo ya Nyumbani Lounge aliweza kualika
ndugu,jamaa na marafiki ili waje kusherekea ushindi wa tuzo hiyo pia bila kusahau
mastaa mbalimbali walijitokeza kwa wingi.
Mchizi Mox,marafiki wa A.yOmmy Dimpoz
Bonny Love akiwa Mchizi Mox
Gerry Rhymes,Mchizi Mox na Gk
Fm kibonde na A.Y
Sunday, December 2, 2012
DHAMIRA NJEMA NI KAMA MTO LAINI, UKIULALIA UNAPATA USINGIZI MARIDADI
"Ndoto yangu ni kuwa Designer" Ndivyo alivyosema kijana huyu yatima anayepata mafunzo Tanzania Mitindo House.
Saturday, December 1, 2012
TUDD THOMAS ATOA SIRI YA MAFANIKIO YAKE
Najua nikizungumzia ma producer wakali katika tasnia hii ya muziki hapa
bongo basi Tudd thomas atakuwa katika list yangu,sasa leo baada ya
kuchonga naye aliweza kunieleza siri ya mafanikio yake katika muziki wa
hapa bongo.Alisema kwamba katika maisha yake atosahau kitu kinachoitwa
ngoma kwani alieleza hizo ndizo zimemfanya hii leo kujulikana katika
tasnia ya muziki na kufanya kazi za wasanii.......... Soma zaidi kwenye Dj Fetty Blog:
Tuesday, November 27, 2012
MSANII SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA
Msanii wa Bongo movie na mwanamziki Sharo
milionea amefariki dunia leo hii kwa ajali ya gari alipokua akielekea
Muheza, Tanga., kwa habari zilizothibitishwa na msanii mwenzake wa movie
Steve Nyerere, akiongea akiwa katika msiba wa msanii mwingine wa Bongo
movie alifariki (John) kwa njia ya simu, akiongea kwa sauti ya
masikitiko sana na Dj Fetty alisema
"ni kweli fetty sharo hatupo nae tena na nimeongea na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga na kuthibitisha habari hizo"
akiongea na Clouds Fm, kamanda wa polisi mkoa
wa Tanga Bwana Constatine Massawe amesema " kifo cha Millionea
kimetokea majira ya saa mbili, eneo linaloitwa Maguzoni songa , akiwa
anaendesha gari aina ya toyota Harrier akitokea Dar kuelekea Muheza,
alipofika hapo gari liliacha barabara na kupinduka,na maiti imehifadhiwa
katika chumba cha maiti ya hospitali teule ya Muheza. alikuwa
mwenyewe. Mungu ailaze roho ya marehem mahali pema peponi Amen.
Saturday, November 10, 2012
MSHINDI WA EPIQ BONGO STAR SEARCH 2012 NI WALTER CHILAMBO
Subscribe to:
Posts (Atom)