UA-45153891-1

Saturday, August 31, 2013

LULU ATOA BURUDANI KALI KWENYE UZINDUZI WA "FOOLISH AGE"


 Lulu na Lady Jaydee

MSANII wa Filamu Bongo, Elizabeth Michael 'Lulu', usiku wa kuamkia leo amefanikisha zoezi la uzinduzi wa filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Foolish Age Tukio la uzinduzi huo lilifanyika katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar, na kuhudhuriwa na mastaa kibao wa tasnia mbalimbali hapa Bongo, wakiwemo; Judith Wambura 'Lady Jaydee', ambaye alitumbuiza sambamba na Barnaba na Amini.


Msanii huyo aliendelea pia kudhihirisha kipaji chake cha kuimba baada ya kuuimba kwa umakini mkubwa, wimbo wa YAHAYA wa Nguli wa muziki wa Kizaki kipya Lady Jaydee na kutunzwa na mapedeshee kibao akiwempo papaa Richie Rich.


Uzinduzi wa fikamu hiyo ya kiswahili ambayo ina sub title ya Kiingereza na ambayo haipaswi kuangaliwa na watoto chini ya miaka 16, huku ikiwa imechezwa na wasanii maarufu na wakongwe  kama Elizabeth Michael mwenyewe, Diana Kimaro, Hashim Kambi, Ombeni Phiri na Mzee Jengua ulifanyika Mlimani City jijini Dar es Salaam.


 Lulu, Mama yake, pamoja na Lady Jaydee
 Lulu na pesa alizotunzwa

Waongozaji wa shughuli hiyo, mtangazaji Double G wa Radio One/ ITV  na mwanadada kutoka Times FM walikuwepo.
 Richie Rich akimwaga noti
Wema Sepetu na Kajala
 Mama na mwanao ni kama chanda na Pete... huyo ni Natasha (kulia) na Bintiye Monalisa.
Mwogozaji wa Filamu za Kibongo, Leah Mwendamseke nae alikuwepo kuangalia kazi hiyo ya Lulu.
 JB Furaha ilitawala 
 Wadau wengi na mashabiki wakifuatilia uzinduzi wa Filamu hiyo

No comments:

Post a Comment