UA-45153891-1

Saturday, August 24, 2013

MWANA FA, DIAMOND, KALA JELEMIAH, MWASITI, LINEX NA WENGINE KURUDI SHULE MWAKA HUU



WASANII kibao wa Bongo Flava na Hip hop  wamegeukia upande wa elimu na kuitizama kwa jicho la tatu kwa kuimba wimbo wa kuhamasisha wanafunzi na wadau mbalimbali wa elimu kufanya kila linalowezekana ili kutokomeza ziro kwenye matokeo ya mitihani ya ngazi mbalimbali  za elimu kuanzia elimu ya msingi.

Wimbo huo ambao umerekodiwa katika studio ya Tudd Thomas Production, umeimbwa na wasanii wasiopungua kumi ambao ni Linex, Mwana FA, Keisha,na Diamond. Wengine ni Roma, Mwasiti, Kala Jeremiah, Petter Msechu, Maunda Zollo, Linah na Baba Levo.

Mwisho wa ziro na elimu bora ni muhimu kwa kila mmoja ni baadhi ya maneno yanayosikika katika wimbo huo unaoitwa TOKOMEZA ZIRO.

No comments:

Post a Comment