UA-45153891-1

Sunday, June 26, 2016

UCHAMBUZI- JINSI YA KUPATA AINA YA MUZIKI INAYOWAKILISHA TANZANIA

Ndugu wasomaji wa  gazeti tanzu hili la semadat, niwaombe radhi kwa kusitisha habari  na makala zangu kwa kipindi cha nyuma kisichopungua mwaka mmoja. Ilikuwa ni katika arakati  zangu za kuendelea kuunganisha vipaji na ujuzi  kama ilivyo kauli mbiu ya maisha yangu yaani “Combining my talents and Skills”. Sasa tunaendelea na leo tunaanza kwa ni jinsi gani inaweza kupatikana aina ya  muziki unaowakilisha nchi ya Tanzania.

Siku moja  niliulizwa na mdau mmoja wa muziki  kwamba “Unauonaje muziki wa Tanzania”, Nikamwambia “Muziki wa Tanzania unakua, unazaa na hivyo unahitaji nafasi au mazingira mazuri ya kulea na kukuza. Linaweza lisiwe jibu lililozoeleka katika masikio ya walio wengi maana katika hili wengi huzungumzia mafanikio ya yanayoonekana kwa mwanamuziki mmojammoja, hamasa kubwa ya wadau vikiwemo vyombo vya habari, makampuni na Taasisi mbalimbali zinavyowekeza katika sanaa hii na kuufanya muziki kuwa biashara na jinsi jamii inavyoupokea na kuukubali tofauti na siku za nyuma. Hii ni sawa kabisa, ni miongoni mwa viashiria vya ukuaji wa sanaa hii.

Lakini tukiuzungumzia muziki wenyewe kiashiria kikubwa  cha ukuaji wake ni jinsi ambavyo unaanza kujitegemea. Katika baadhi ya nchi kama Afrika kusini na Nigeria, sio kwamba hakuna aina zingine za muziki nchini humo kama nchi ya Tanzania ilivyo na Muziki wa Dansi, Mchiriku au Mnanda, Taarabu na zingine nyingi zikiwemo za asili kama ile ya Saida Karoli. Kilichotokea katika nchi hizo ni kwamba, zilijitokeza aina zingine za muziki ambazo ziliakisi muziki wa Amerika na Ulaya kwa muda lakini baadae zikarudi nyumbani kwao. Hapo ndipo ikapatikana Kwaito ya Africa Kusini na ile inayoitwa Niger Style ya Nigeria.
Nimetumia nchi hizo mbili kama kiwakilishi kwa nchi zingine za Afrika ambazo zimefikia hatua hiyo na kwa kuwa huo ndio muziki wa kizazi kipya wa nchi hizo sasa nirudi katika muziki wa kizazi kipya wa Tanzania yaani “Bongo Flava”.

Ninapozungumzia muziki wa Tanzania kwa sasa nazungumzia muziki huu wa kizazi kipya  lakini kwa kuhusisha aina zilizokuwepo kabla ya Bongo Flava, ambazo baadhi nimezitaja ndipo narejea katika  mambo matatu ambayo ni kukua, kuzaa na kukuza.

Katika maisha ya kawaida kifamilia, mtoto anapokuwa mkubwa anaondoka nyumbani, lakini kimuziki mtoto anapokuwa mkubwa anarudi nyumbani.
Ikumbukwe kwamba Muziki huu wa kizazi kipya, ulianza kwa kuakisi aina mbili za muziki wa Marekani ambazo ni Hip-Hop na RnB. Lakini leo muziki huu umerudi Afrika, ndiyo maana vionjo vinavyotawala katika muziki huu ni Afro beat, Afro Pop, Zouk, Rumba, Chacha na zingine nyingi za hapa hapa Afrika. Hiyo ni hatua ya kwanza katika kukua kwa muziki huu.
Hatua inayofuata ni muziki huu kurudi hapahapa nchini Tanzania kwa maana ya kuakisi muziki uliyokuwepo awali. Hiyo imeshaanza kutokea. Tunashuhudia msanii maarufu kama Diamond Platnumz akiunganisha muziki wake na mitindo ya Taarabu (Mduara), Mnanda na nyinginezo. Sikiliza pia kwa makini vionjo vya muziki anaofanya AY kwa sasa. Wapo pia ambao wameanza kuuchanganya na midundo, melodia na lugha za asili kuufanya muziki huu kuwa wa kitanzania zaidi.

Kwa Muziki huu  kurudi nchini Tanzania, zinajitokeza aina flani za muziki ambazo  siyo Bongo Flava ya miaka ya 1990-2000. Hao ndio watoto wanaozaliwa ambao wanatakiwa kulelewa. Watoto hao ndiyo watatupa aina ya  Muziki itakayotutambulisha. Kadiri watoto hao wanavyozidi kuwa wengi kila mmoja atakuwa akileta hamasa kwa mwingine na  tabia zao kufanana na hatimaye kufanya kitu kimoja. Hiyo ndiyo itakuwa hatua ya ukomavu.

Kuna mijadala na maswali kwamba aina ya muziki inayoitambulisha Tanzania ni ipi, kwa kuwa hata “Bongo Flava” siyo aina  ya muziki, bali jina linalowakilisha aina mbali mbali za muziki wa kizazi kipya. Kweli itaendelea kuwa hivi. Inaweza kuchukua hata zaidi ya muhongo mmoja kuanzia sasa, lakini kwa kupitia hatua hizo ambazo zimeshaanza kujitokeza itakapofika  hatua hiyo ya ukomavu ndipo kitapatika kile kinachofahamika kama ‘Identity’ ya muziki wa Tanzania.

Wednesday, April 2, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AZUNGUMZIA KAMPENI YA KILIMO YA ONE.ORG INAYOITWA'Do Agric'


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz ambaye ni miongoni mwa wanamuziki 19 wa Afrika waliochaguliwa kukutana  nchini Nigeria ili kushiriki katika wimbo wa pamoja wa kuhamasisha vijana kujiunga na kilimo, amesikika akizungumzia kampeni hiyo leo kupitia Clouds FM. 

"Kilimo si ushamba, tajiri wa kwanza Afrika Aliko Dangote ni mkulima pia. Unaweza kuwa na shughuri zako mjini lakini ukawa mkulima pia kupitia watu uliowaajiri ambao wanafanya kazi moja kwa moja shambani, inawezekana pia kwa watu kama sisi ambao wengine wanatuita wauza sura", alisema Diamond ambaye pia akiwa jijini Lagos, amefanikiwa kumalizia wimbo wake anaofanya na staa wa nchini humo 'Iyanya' ambaye alikuwa hapa nchini Tanzania mwaka jana katika msimu wa Fiesta.

MR NICE BADILI MATUKIO HASI KUWA CHANYA



Sina uhakika kama uko facebook, twitter, Insatagram au kwingine niweze hata kushauri chochote kupitia akaunti yako. Labda tu niseme kupitia semadat, sina shaka waweza pata ujumbe huu kupitia watu wengine ambao uko karibu nao na wako mtandaoni. Kaka  umaarufu wako ni mkubwa sana. Mpaka mwanzoni mwa mwaka jana, wewe na  Saida Kalori ndiyo wasanii pekee wa muziki wa Tanzania mliokuwa mkitolewa mifano mpaka na viongozi wataalam wa masoko katika mada mbalimbali za nembo au alama  mashuhuri za watu kwa kuzungumzia mtu mmoja mmoja au kwa lugha ya Kiingereza wanasema 'Personal Branding'.

TUNDAMANI ATAKIWA KUWA MZALENDO


Wakati vyombo kadhaa vya habari vikihubiri Uzalendo na Amani, msanii wa Bongo Flava ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Msambinungwa, ameonekana kuwa tofauti baada ya mwanadada mmoja anayeitwa Esta kuweka wazi kwamba picha za video ya wimbo huo hazikuchukuliwa  jijini Nairobi kama mwanamuziki huyo alivyosema, bali shughuri hiyo ilifanyika hapa hapa nchini Tanzania kwenye studio inayoongozwa na mwanadada huyo mjasiliamali. 

Tuesday, April 1, 2014

RAMANI YA DUNIA KAMA ILIVYOKUTWA MTANDAONI


BONGO QUEEN LEO NDANI YA SEMADAT

Leo tuko na muimbaji katika muziki wa kizazi kipya yaani  Bongo Flava ambaye anaitwa Linah Sanga. Anatokea katika nyumba ya vipaji THT. Huwezi kuwataja waimbaji bora wa kike nchini Tanzania pasipo kumtaja. Yuko katika tuzo za KTML 2014 kipengele cha muimbaji bora wa kike.

SEMADAT NA WAWILI KWA PICHA- JACKLINE WOLPER NA JOKATE MWEGELO


AGNES GERALD 'MASOGANGE' KUSHIRIKI VIDEO MPYA YA 50 CENT NCHINI MAREKANI


Muigizaji maarufu wa video za muziki 'video vixen' wa hapa Tanzania, Agnes Gerald 'Masogange' ataondoka kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki kwenye video mpya ya mwanamuziki mahiri wa Hip hop nchini Marekani '50 Cent'. Mwanadada huyo ambaye amefanya video za wanamuziki kadhaa wa hapa nchini ikiwa pamoja na za nyimbo kama 'Masogange' wa Belle 9 na 'Nangoja ageuke' wa Mwana FA, ameitwa nchini Marekani kwa ajili ya shughuri hiyo baada ya kuonekana kupitia mtandao wa kijamii wa Youtube kwenye moja ya video za muziki wa Bongo Flava.

Agnes Gerald katika picha zaidi:

Thursday, March 27, 2014

HAPPY BIRTHDAY MARIAH CAREY


Staa huyu wa "We Belong Together" ametimiza miaka 44 leo.

GARI ALILONUNUA MASANJA MKANDAMIZAJI


Mchekeshaji hodari hapa nchini Tanzania maarufu kama 'Masanja Mkandamizaji' ambaye ni miongoni mwa watanzania waliofanikiwa kupitia sanaa, amenunua gari hili, kama linavyoonekana kwenye picha hapa chini.