TUDD THOMAS PRODUCTION COMPANY LIMITED tunaungana na watanzania wote kuomboleza msiba wa Mangwea na pia tunawapa pole ndugu, jamaa na marafiki!!! KATIKA MUNGU TUNAAMINI!!!
.
Friday, May 31, 2013
SALAAM ZA PRODYUZA TUDD THOMAS JUU YA MSIBA WA ALBERT MANGWEA
TUDD THOMAS PRODUCTION COMPANY LIMITED tunaungana na watanzania wote kuomboleza msiba wa Mangwea na pia tunawapa pole ndugu, jamaa na marafiki!!! KATIKA MUNGU TUNAAMINI!!!
HISTORIA YA MAREHEMU ALBERT NGWAIR
JINA LAKE HALISI NI ALBERT KENETH
MANGWAIR,NI MTU WA RUVUMA MNGONI...,,,,MNGONI,LAKINI ALIZALIWA MBEYA
TAREHE 16 NOVEMBER,MWAKA 1982.YEYE NI MTOTO WA MWISHO KWAO,KWA BABA
AKIWA MTOTO WA 10,KWA MAMA AKIWA MTOTO WA 6.
NGWAIR ASILI YAKE NI RUVUMA,YAANI
MNGONI, ALIZALIWA MBEYA,A KIWA MIAKA 5 WALIHAMIA MOROGORO AKASOMA
SHULE YA MSINGI BUNGO HADI DARASA LA 5, BABA YAKE AKAPATA UHAMISHO
AKAHAMIA DODOMA, AKAHAMA NA BABA YAKE AKAENDA KUMALIZA SHULE YA
MSINGI MLIMWA DODOMA. KISHA MAZENGO SEC, NA BAADAE CHUO CHA UFUNDI
MAZENGO.
Thursday, May 30, 2013
MWANA FA, AAHIRISHA SHOW YAKE YA "THE FINEST" KWA HESHIMA YA NGWAIR.
Kwa heshima ya Ngwea, Mwana FA ametangaza kuahirisha show yake y The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013. |
Kutokana
na habari za kufariki kwa mwanamuziki Albert Mangwair, msanii ambaye ni
mmoja kati ya wana Hip Hop maarufu nchini, Mwanamuziki mwingine pia wa
Hip Hop Hamis Mwin'jumah, a.k.a MwanaFA(Pichani)nametangaza kuahirisha
show yake ya The Finest iliyokuwa ifanyike Ijumaa hii May 31, 2013.
HABARI; www.jestina-george.com
ALICHOKIANDIKA LADY JAYDEE KUHUSU KUAHIRISHA SHOO YAKE YA MIAKA 13 BAADA YA KIFO CHA NGWAIR
Tunaomba radhi kwa watu wote ambao mlikuwa mmeshanunua tickets za miaka 13 ya Lady Jaydee ambapo onyesho ilikuwa lifanyike Ijumaa ya tar 31 Mei 2013.
Tunapenda kuwataarifu kuwa onyesho hilo limesitishwa kutokana na msiba mzito wa msanii mwenzetu Ngwair mpaka hapo tutakapo wataarifu tena.
Tunasubiri taratibu za kuupokea mwili na tarehe ya maziko, baada ya hapo tutaendelea na ratiba za show na tutawatangazia tarehe inayofuata ambayo si mbali baada ya maziko.
Wale mliokwisha nunua tickets naomba mzitunze tickets zenu, kwani ndio hizo hizo mtakazozitumia siku ya show hata kama tarehe imebadilishwa.
Natanguliza shukrani na naomba radhi kwa usumbufu wowote nitakaokuwa nimewasababishia.
Kila kitu kitaendelea kama kilivyokuwa kimepangwa, hapo baadae.
Tuesday, May 28, 2013
R.I.P ALBERT MANGWAIR
Albert Mangwair a.k.a Mimi a.k.a Ngwair.
Albert Mangwair a.k.a Mimi a.k.a Ngwair alikuwa msanii wa Hip Hop ya Bongo kutoka mkoani Dodoma. Mwaka 2003 Ngwair alikutana na mtayarishaji mahiri wa muziki P Funk Majani na kuanza kufanya naye kazi ambapo alitoa kibao cha kwanza kiitwacho 'Ghetto Langu,' nyimbo iliyompatia umaarufu mkubwa. Mangwair pia aliwahi kushinda tuzo ya Kilimanjaro Music Awards kama mwana Hip Hop Bora wa mwaka 2005. Mwaka wa 2007 akatoka kwa wimbo wa Kimyakimya akiwa na Wana Chemba Squad.
Habari zaidi na Globalpublishers.info
Saturday, May 25, 2013
MZOZO WA JACQUELINE WOLPER NA BABY MADAHA
SIKU chache baada ya wasanii wa filamu Bongo, Jacqueline Wolper na Baby Madaha kuingia kwenye mzozo wa kugombea nyumba moja ya kupanga ambayo wote waliilipia kodi kwa nyakati tofauti, bifu zito linalotajwa kuwa ni la kifo limeibuka.
Jacqueline Wolper.
Sakata la wawili hao lilifika polisi na kubainika kuwa Madaha alilipa kodi kwa tapeli wakati Wolper alitoa fedha zake kwa mwenye nyumba hivyo kumfanya awe na haki ya kuhamia.
Akizungumza na Ijumaa, juzi jijini Dar es Salaam, Madaha alisema pamoja na kubainika kuwa alitapeliwa, mtu pekee ambaye angeweza kumsaidia kupata fedha zake (shilingi milioni tatu) ni Wolper lakini anamchenga.
MADAI YA MADAHA
“Ni kweli nimetapeliwa lakini Wolper kama msanii mwenzangu alikuwa na uwezo wa kunisaidia maana yeye anaishi pale lakini nimemwambia, ananipiga chenga. Sitaongea naye milele, hana utu kabisa. Milioni tatu ndugu yangu si pesa ndogo.”
Baby Madaha.
HUYU HAPA WOLPER
Wolper alipotafutwa na Ijumaa na kusomewa malalamiko ya Madaha alisema: “Naweza kusema Madaha hana akili, ni mpuuzi kwa sababu angekuja kwa busara nyumbani kwangu tungezungumza na baba mwenye nyumba tukajua namna ya kumsaidia.
“Lakini yeye kabla hajaomba ushirikiano kwangu, tayari naanza kusumbuliwa na magazeti kuwa eti nimemtapeli. Halafu hajawahi kunipigia simu bali alikuwa anawatuma watu wake kwangu. Kwa nini asingekuja mwenyewe?
“Ina maana yeye ni staa sana au? Huyu hana lolote anataka kupanda kwa kutumia jina langu,” alisema Wolper.
Habari na Gladness Mallya wa GLOBAL PUBLISHERS
Tuesday, May 21, 2013
TUDD THOMAS KUWAREKODIA WIMBO WASHINDI WA THE VODACOM MIC KING
Majaji wa Shindano la The Vodacom Mic King, kutoka kushoto ni John Dilinga Mathlou (JD), Abdallah Mrisho (Abby Cool) wa Global Publishers na Producer Ally Baucha wa Baucha Records.
Pembeni mwa majaji, kushoto ni msanii wa Hip Hop, Stamina na kulia ni Producer Tudd Thomas, nyuma ni washiriki wa shindano hilo.
Waandishi
wa habari na wageni wengine
Washiriki wa shindano la The Vodacom Mic King na gari atakalopewa mshindi
MSHINDI wa kwanza, wa pili na wa tatu wa shindano la The Vodacom Mic King linaloandaliwa na uongozi wa Dar Live chini ya udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom, watapata fursa ya kurekodi wimbo mmoja chini ya producer mahiri nchini Tudd Thomas, aliyerekodi wimbo maarufu wa Leka Dutigite wa Kigoma All Stars na nyingine nyingi.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Atriums Mei 21, 2013, meneja matukio wa Dar Live Bw. Abdallah Mrisho amesema, jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi wa kwanza ataondoka na gari aina ya TOYOTA FUNCARGO (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Tamasha la shindano hili litafanyika Mei 25, 2013 katika uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem au kwa jina linguine Mbagala Rangi Tatu.
Majaji katika shindano hilo ni DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou (JD), Producer Ally Baucha kutoka Baucha Records na mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho au Abby Cool wa Kampuni ya Global Publishers. Shindano hili ni la muziki wa Kurap au Hip Hop ambalo lina lengo la kuwaendeleza vijana wenye lengo la kufanya muziki katika maisha yao.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Atriums Mei 21, 2013, meneja matukio wa Dar Live Bw. Abdallah Mrisho amesema, jumla ya vijana tisa wenye vipaji watapanda stejini kuchuana na mshindi wa kwanza ataondoka na gari aina ya TOYOTA FUNCARGO (New Model) yenye thamani ya shilingi milioni 15. Tamasha la shindano hili litafanyika Mei 25, 2013 katika uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem au kwa jina linguine Mbagala Rangi Tatu.
Majaji katika shindano hilo ni DJ mkongwe nchini, John Dilinga Matlou (JD), Producer Ally Baucha kutoka Baucha Records na mwandishi mkongwe wa habari za muziki na wasanii, Abdallah Mrisho au Abby Cool wa Kampuni ya Global Publishers. Shindano hili ni la muziki wa Kurap au Hip Hop ambalo lina lengo la kuwaendeleza vijana wenye lengo la kufanya muziki katika maisha yao.
Stamina, Tudd Thomas na mmoja wa waandishi wa habari baada ya mkutano.
Tudd Thomas, John Dilinga (JD), Stamina na Ally Baucha
Dat (Mwandishi wa nyimbo,
matangazo na Blogger wa datsongwritertz Blog) akiwa na Tudd Thomas muda mfupi baada ya mkutano na waandishi wa habari
Monday, May 20, 2013
KINACHOMPONZA TUDD THOMAS NI UCHAWI AU KUSAHAU?
t Tudd Thomas
MASHABIKI wa mtayarishaji wa muziki (Producer), mwenye uwezo wa kipekee, aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars na zingine nyingi, Tudd Thomas, wamekuwa wakiulizana maswali mengi wao kwa wao pasipo kupata majibu.
MASHABIKI wa mtayarishaji wa muziki (Producer), mwenye uwezo wa kipekee, aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars na zingine nyingi, Tudd Thomas, wamekuwa wakiulizana maswali mengi wao kwa wao pasipo kupata majibu.
Safari ya Tudd Thomas katika muziki, ilianzia mkoani Iringa akiwa Iringa Records aliporekodi wimbo wa mwanamuziki Marlaw unaoitwa Bembeleza. Wimbo huo ulipata tuzo ya wimbo bora wa mwaka kutoka Kilimanjaro Tanzania Music Awards mwaka 2008 na pia kumfanya Marlaw apate tuzo ya msanii bora wa kiume kupitia tuzo hizo. Baadae alihamia jijini Dar es Salaam na ndipo alipoonesha uwezo wake zaidi kwa kusuka nyimbo zilizotikisa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.
Hakuna hasiyeufahamu wimbo wa Pii, Pii (Missing my baby) wa Marlaw ambao aliutengeneza yeye kupitia Studio ya JML. Wimbo huo ulipata tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na tuzo ya Nzumari nchini Kenya mwaka 2009 mbapo uliingia kwenye kipengere cha wimbo bora wa Afrika Mashariki, kumfanya Marlaw aingie kwenye kipengele cha msanii bora wa Afrika Mashariki na kunyakua tuzo hiyo. Baada ya hapo wimbo huo ulipata tuzo ya Kilimanjaro nchini Tanzania kama wimbo bora wa mwaka wa Afro pop mwaka 2010, tuzo ya Chaguo la Teneez Music nchini Kenya kama wimbo ulioongoza kwa kuchukuliwa kwa njia ya mtandao Afrika Mashariki “The most downloaded East African song” mwaka 2010, pamoja na tuzo ya Nigeria Sound City Video Music kama wimbo bora wa Afrika Mashariki mwaka 2010.
Aliendelea kutayarisha nyimbo amabazo zilipata umaarufu mkubwa na kuingia kwenye vipengele mbalimbali vya tuzo za muziki za Kilimanjaro. Mwaka 2012, nyimbo tatu zilizotokana na mikono yake zilipata nafasi ya kushiriki tuzo hizo. Nyimbo hizo ni Liz One wa Izzo Business ambao uliingia kwenye vipengele viwili ambavyo ni wimbo bora wa mwaka na wimbo bora wa Hip hop na pia kusababisha msanii huyo aingie kwenye kipengele cha msanii bora wa Hip hop. Milele daima wa Barnaba na Kizunguzungu wa Rachel, ambapo zote ziliingia kipengele cha wimbo bora wa Zouk/Rhumba pia ni nyimbo alizotengeneza mtayarishaji huyo.
Nyimbo zingine alizotayarisha ambazo zilifanya vizuri kwenye vituo mbalimbali vya redio na TV ni Kisa pombe na Soldier za Mwasiti, Sorry sana, Mbayuwayu na Mtoto wa Afrika za Marlaw pamoja na Natumaini ya Becka aliyowashirikisha Barnaba na Amin. Pia zipo nyingine kama Unikimbie ya Amin, Tushukuru kwa yote ya Ditto, Lonely ya Linah na Magubegube ya Barnaba.
Mtayarishaji huyo ambaye hajawai kuingia kwenye tuzo za Kilimanjaro za muziki wa hapa nchini Tanzania ambazo mwaka huu zimeongezewa kipengele cha Mtayarishaji bora chipukizi ndiye aliyetayarisha wimbo wa Leka dutigite wa Kigoma All Stars kupitia Studio yake ya Ngoma Records. Wimbo huu umeingia kwenye kipengele cha wimbo bora wa mwaka 2013. Pia alishirikiana na mtayarishaji Imma the boy kutengeneza wimbo wa Me ‘n’ U wa Ommy Dimpoz ambao umeingia kwenye kipengele hicho na vipengele vingine ambavyo ni wimbo bora wa Bongo Pop na wimbo bora wa kushirikiana.
Alipoulizwa alisema hapendi kuzungumzia juu ya kutotajwa kama miongoni mwa wanaowania tuzo. Aliendelea kusema kwamba, hata kama baadae ikitokea, kwake ni motisha tu, lakini kikubwa zaidi ni kwamba anahisi analo deni kubwa la kutumia uwezo wake ipasavyo kufanya kazi nzuri zaidi ya hapo ili kuutangaza muziki wa Tanzania kimataifa. Pia alisema ana malengo makubwa aliyojiwekea na ndiyo maana kila kukicha anawaza kutayarisha nyimbo zenye tofauti na zenye ladha ya kipekee.
Tudd Thomas anaendelea kukitumia kipaji chake na ujuzi wake ipasavyo na siku chache zilizopita kuna nyimbo zisizopungua tatu zilizoingia sokoni na zinafanya vizuri, ambazo ni kazi za mikono yake. Nyimbo hizo ni Uswazi take away ya Chegge, Nyumbani ya Kigoma All Stars na pia ameshirikiana kwa kiasi kikubwa na mtayarishaji Fundi Samwel kutengeneza wimbo wa Mahakama ya mapenzi wa Linex.
Sunday, May 12, 2013
TAMASHA LA KAMPENI YA TWENDE ZETU UWANJA WA JAMHURI MJINI DODOMA
Wakazi wa Mji wa Dodoma na vitongoji vyake wakiwa wamefurika kwa wingi
katika uzinduzi wa msimu mpya wa Clouds FM uliofanyika katika uwanja
wa Jamhuri mjini humo.
Shilole
Rich Mavoko
Timbulo
Dogo Asley
KILICHOJIRI HUKO DODOMA KWENYE SEMINA YA TWENDE ZETU YA CLOUDS MEDIA GROUP
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds FM Bw. Ruge Mutahaba akizungumza katika semina hiyo .
Mh. Zitto Kabwe akiingia katika ukumbi wa mikutano wa African Dream mjini Dodoma.
Mtoa mada Patrick Ngowi akiingia kwenye ukumbi wa mkutano
Msanii Mrisho Mpoto ambaye pia ametoa mada katika semina hiyo
Mtoa mada Zeno Ngowi akizungumza na wasanii katika semina hiyo.
Millad Ayo akizungumza kulia ni Dina Mario na Zamaradi Ntetema
Mkubwa Fella kutoka TMK akizungumza katika semina hiyo
Anold Kayanda akitoa mawazo yake.
Dj fetty
Gerlad Hando
Khamis Mandi B12 akichangia Mada
DJ Elly katikati Godzilla kushoto na Izo Busness wakiwa katika semina hiyo.
Afande Sele katikati na rafiki yake wakiwa na Shilole
Benny Kinyaiya akizungumza katika semina hiyo kulia ni Babu Tale na kushoto ni Said Bonge.
Shafii Dauda na Diva wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa katika semina hiyo
Ibrahim Masoud na washiriki wengine wakiwa katika semina hiyo
Saturday, May 11, 2013
SNURA NA SHILOLE MAJANGA
MWANAMUZIKI na muigizaji wa kike Snura Mushi
'Snura', ametumia zaidi ya dakika 45 kuzungumza na mashabiki wake juu ya ugomvi
wake na Zuwena Mohamed 'Shilole' ambaye pia ni mwanamuziki na muigizaji.
Mwanadada huyo anayetamba na wimbo wa “Majanga” ambao kwa sasa ndiyo habari ya
mjini kwenye vituo mbalimbali vya redio na mitaani, alisema Shilole amekuwa
akimtuhumu kuwa kaiga staili yake ya uimbaji.
Snura kupitia Amplifier ya Clouds FM juzi, alisikika akisema staili yake ya uimbaji ni tofauti kabisa na ile ya Shilole. Alifafanua kwamba Shilole anaimba staili ya mduara wakati yeye hafanyi muziki wa aina hiyo ingawa hakuweka bayana aina ya muziki anayoifanya yeye. Aliendelea kusema kwamba Watanzania wanaweza kuwafananisha yeye na Shilole kama waigizaji wa kike ambao pia ni wanamuziki, lakini sio kwa aina ya muziki waufanyao. Pia alisisitiza kuwa, tofauti ya aina zao za muziki ni kama Marekani na Chanika.
Subscribe to:
Posts (Atom)