UA-45153891-1

Tuesday, December 17, 2013

BEYONCE KUWASHINDA KATY PERRY NA LADY GAGA, ALBUM YAKE MPYA KUUZA NAKALA ZAIDI YA 600,000 NDANI YA WIKI MOJA



Beyonce

Album mpya ya Beyonce  imefanya maajabu sokoni baada ya kuuza nakala 430,000 baada ya siku moja na masaa machache tangu ilipoingia sokoni Alhamisi ya wiki iliyopita. Album hiyo inayoitwa ‘Beyonce’ ambayo iliingia sokoni bila taarifa kwa kile kinachotajwa kuwa ni ‘surprise’,inatarajiwa kushika namba 1 kwenye chart za Billboard na ina  uwezekano mkubwa kuuza nakala zaidi 600,000 kufikia Jumanne  na kuwa Album ya kwanza kwa mauzo kwa wanamuziki wa kike mwaka huu 2013 ikilinganishwa  ‘Prism’ ya Katy Perry iliyouza nakala 286,000 wiki nzima, ‘Artpop’ ya Lady Gaga nakala 258’000 na ‘Bangerz’ ya Miley Cyrus nakala 270,000 wiki nzima.

Kama Beyonce atafikia mauzo ya nakala 600,000  itakuwa ni wiki ya mauzo makubwa zaidi  kwake katika album zote alizowai kutoa. Mwaka jana 2012, aliyeongoza kwa wanamuziki wa kike ni Taylor Swift kupitia album yake ya ‘Red’ iliyouza nakala millioni 1.2 . Album mpya ya Beyonce  ambayo kwa sasa inapatikana i-tune, ina nyimbo 14 zote  pia zikiwa ni video.

No comments:

Post a Comment