Soko la mitandao ya kijamii ulimwenguni linazidi kukua ambapo mpaka sasa zaidi ya watu bilioni 1.73 wanaitumia. Kwa mujibu wa mtandao wa “eMarketer” unaofuatilia kwa ukaribu zaidi masuala hayo, idadi hiyo inatarajiwa kufikia billion 2.5 ifikapo mwaka 2017 na kuna mambo mengi yatajitokeza mwaka ujao wa 2014. Yafuatayo ni baadhi ya mambo yatakayotokea.
1. Twitter itakuwa juu ya FacebookT
afiti mbalimbali zinaonyesha idadi ya vijana kuanzia umri wa miaka 13-17 wanahama kutoka facebook kwenda twitter na Instagram ili kuwakimbia wazazi na walezi wao ambao wamekuwa wakijiunga kwa lengo la kufuatilia wayafanyao. “Because there is less drama and it’s also easier to fly without parents”, Alisema kijana mmoja. Kwa upande wa ‘Brands’ makampuni mengi tayari yanatumia Facebook na Twitter lakini makampuni mengine kama ya Hoteli, Utalii, Usafiri n.k, kama ikitokea kampuni flani katika biashara hizo, iko katika mtandao mmoja kati ya hiyo, mara nyingi utaikuta Twitter. Twitter ni mtandao unaotajwa zaidi kwa kupewa kipaumbele katika shughuri za huduma kwa wateja.
2. Google+ itaanza kufanya maajabu
Kama ijulikanavyo kwamba Google ndiyo ‘Brand’ inayoongoza, siyo tu kwenye tovuti za Dunia, bali katika kila kitu, wanakuja na mikakati kabambe ya kufanya mtandao wao wa kijamii wa Google+ kuwa na sifa zote nzuri za kufanya kila mtu hasione sababu ya kutouchagua kwa matumizi ya kibiashara au matumizi binafsi.
3. Biashara kuwekeza kwenye mitandao ya kijamii itakuwa lazima si chaguo
Kwa yule ambaye kweli anahitaji kushindana kibiashara atalazimika kutumia eneo hili kama sehemu ya mikakati ya kimasoko. Makampuni mengi yatatangaza nafasi za kazi kutafuta watu maalum kwa ajili ya shughuri za kusimamia mitandao ya kijamii pamoja na kuyatumia makampuni na mawakala wanaotoa mafunzo juu ya matumizi ya mitandao hiyo.
4. Mitandao ya kijamii itatumika zaidi kuonyesha kuliko kusema
Matumizi ya picha na video yataongezeka zaidi ya maandishi, hivyo umaarufu wa mitandao kama Instagram na Pinterest utaongezeka hasa katika matumizi ya matangazo. Makampuni yataanza kutayarisha video maalum na fupi zinazojulikana kama ‘Micro- video’ kwa ajili ya mitandao ya kijamii. Kama ilivyo kwenye vyombo vya habari kama Televisheni ambapo tangazo la biashara linatakiwa kuwa sekunde zisizozidi 60 kwa mfano, na mitandao ya kijamii ina muda maalum wa video inayotakiwa kuingia humo. Mfano katika Instagram ni sekunde zisizozidi 15. Hivyo makampuni yatakuwa na kazi ya kuandaa matangazo mafupi kwa ajili hiyo na yenye kutoa ujumbe kamili sawa na yale ya Televisheni.
5. Taarifa maalum na kwa malengo maalum ndani ya mitandao zitatawala zaidi
Mitandao itatumika zaidi kwa ajili ya taarifa kubwa kubwa zenye malengo maalum kama kuelimisha na kuhabarisha “Micro-bloging” badala ya majibizano “Conversation”. Mfumo wa majibizano utabaki kwenye ile mitandao inayotumika zaidi kwenye simu ambayo inaitwa ‘Apps’ na ‘Messenger’, mfano Snapchat, Whatsup na mingineyo kwa ajili ya kuchat. Ni moja ya mambo yanayoifanya Twitter izidi kuvuta watu kutokana na kutumika kama Micro-blog mbali na matumizi yake ya ‘tweets’ kama ujumbe mfupi wa maneno.
No comments:
Post a Comment