UA-45153891-1

Thursday, December 19, 2013

VIMBWANGA VYA TWITTER KUFANYIWA MAIGIZO YA TELEVISHENI

Kitabu  kinachoitwa ‘Hatching Twitter’ kilichoandikwa na mwandishi wa gazeti la New York Times la nchini Marekani anayeitwa Nick Bilton, kitatumika kutayarisha kipindi cha tamthilia cha Televisheni ambacho kitaanza kuruka hewani katika mtindo wa ‘series’.

Kitabu cha‘Hatching Twitter’


Kitabu hicho ambacho kinazungumzia stori ya kweli inayohusu  pesa, nguvu, urafiki na usaliti vikihusishwa na mtandao wa Twitter, kiliingia sokoni mwanzoni mwa mwezi Novemba 2013 na kupendwa sana na wasomaji. Ikiwa sasa  kina mwezi mmoja tu, kimechaguliwa na Televisheni ya Lionsgate kuwekwa katika mfumo huo wa maigizo ambapo stori yake itaanza kufanyiwa kazi ndani ya Hollyhood. Mwandishi wa kitabu hicho Nick Bilton, ndiye anatarajiwa kuandika matukio harisi ya stori hiyo yaani ‘screen play’ na ndiye atakayepata sifa ya utayarishaji.

 Mwandishi wa kitabu cha ‘Hatching Twitter’ Nick Bilton ambaye pia ni mwandishi wa New York Times upande wa habari zinazohusu Teknolojia.

Akizungumza na waandishi wa habari, mwenyekiti wa Televisheni ya Lionsgate Kevin Beggs, amesema mtandao wa Twitter  umebadilisha maisha ya watu wengi kisiasa, kibiashara na kirafiki hivyo amevutiwa na kuamua kuiweka stori ya kitabu cha Bilton katika hali ya muonekano katika TV haraka iwezekanavyo. “Kitabu cha Nick kina kila namna ya hali ya maigizo na hasa kwa jinsi alivyowapanga wahusika katika kuonyesha nguvu ya mapambano na usaliti wa urafiki”, alisisitiza  Kelvin, mwenyekiti wa Lionsgate TV.

Mwenyekiti wa Televisheni za Lionsgate Kevin Beggs (Kushoto) akiwa na Bi. Weeds ambaye ni mbunifu katika masuala ya vipindi vya Televisheni

No comments:

Post a Comment