UA-45153891-1

Tuesday, December 3, 2013

OMOTOLA, UHURU KENYATTA NA P-SQUARE WATAJWA MIONGONI MWA WATU 100 WENYE USHAWISHI MKUBWA BARANI AFRIKA MWAKA 2013

Omotola Jalade

Jarida la Afrika linalojulikana kama ‘New African Magazine’ ambalo hutangaza watu 100 wenye ushawishi mkubwa barani Afrika kila mwaka“100 most influential Africans” , liliwataja watu hao kwa mwaka huu mwishoni mwa Novemba 2013 ambapo miongoni mwao ni muigizaji wa kike wa nchini Nigeria Omotola Jalade, Raisi wa Kenya Uhuru Kenyatta na wanamuziki wa nchini Nigeria Peter na Paul wa kundi la P-Square.

Uhuru Kenyatta

Jarida hilo ambalo lilisisitiza kwamba ushawishi huo haumaanishi kuwa maarufu na si watu wote maarufu wana ushawishi, bali kinachozungumziwa ni jinsi ambavyo watu hao wanaleta hamasa kubwa kwa watu wengine kutokana na mchango mkubwa walionao katika makundi mbali mbali ya kijamii.

P-Square

Watu hao 100 ambao ni kati ya watu zaidi ya bilioni moja katika bara la Afrika kutoka nchi 54, wamegawanywa katika vipengele ambavyo ni Siasa na mashirika ya kimataifa, Biashara, Jumuiya za kiraia, Sayansi na Taaluma kwa ujumla, Dini na mambo ya kiasili, Vyombo vya habari, Sanaa, Utamaduni na michezo. Idadi kubwa ya watu hao kwa  vipengele ilikuwa upande wa Biashara ambapo wameingia watu 33, ikifuatiwa na Siasa watu 20 pamoja na Sanaa na Utamaduni watu 17.Kiujumla nchi iliyoongoza kwa kuwa na watu wengi ni Nigeria ikiwa na idadi ya watu 23, ikifuatiwa na Afrika kusini watu 22 na Kenya watu 9.

Wengine  kwenye orodha hiyo ni pamoja na Don Jazzy ambaye ni mtayarishaji wa muziki nchini Nigeria, Raisi mstaafu wa Afrika Kusini Thabo Mbeki, Bilionea Aliko Dangote wa Nigeria, Msimamizi wa  Ernst and Young  nchini Ethiopia Zemedeneh Negatu, akiwa ndiye pekee kutoka nchini humo, Mwanamuziki D’Banj wa Nigeria na mchezaji wa soka Adebayo wa nchini Togo. Idadi ya wanawake ni 32 ambapo kati yao ni pamoja na Zuriel Oduwole mwenye umri wa miaka 11 ambaye ni mwanaharakati mdogo anayepigania elimu ya wanawake barani Afrika akitokea nchini Nigeria.
Zuriel Oduwole (Miaka 11)

No comments:

Post a Comment