UA-45153891-1

Friday, November 29, 2013

MBUNIFU STEPHEN JONES ATENGENEZA NGUO ZA 'CHRISTMAS' KWA AJILI YA WANASESERE AINA YA BARBIE

Mwanasesere aina ya Barbie

Wakati wabunifu mbalimbali wa mavazi ulimwenguni wakiendelea kuleta mitindo mipya katika tasnia hiyo, mbunifu wa mavazi ya wanawake Stephen Jones ambaye ni muingereza anayefanyia shughuri zake jijini London, amekuza soko lake kwa kuanza kutengeneza mavazi ya wanasesere  ambao kwa  lugha ya kiingereza  wanaitwa ‘Dolls’. 

Kwa kuwa kuna aina zaidi ya moja katika maumbo ya wanasesere, Stephen amechagua kutengeneza mavazi ya wanasesere aina ya Barbie. Ametoa toleo lake la kwanza la mavazi maalum kwa ajili ya msimu wa sikukuu ya ‘Christmas’ ya mwaka huu 2013.


Barbie ni mwanasesere mwenye umbo kubwa  aliyebuniwa mwaka 1959 na mfanyabiashara mwanamke wa kimarekani anayeitwa Ruth Handler . Ilitokea baada ya kumuona mtoto wake wa kike  anayeitwa Barbara akitamani mwanasesere aliyekuwa nae awe mkubwa  kama  mtoto  wa zaidi ya miaka mitano badala ya kumuona  siku zote akiwa kama mtoto mchanga. Ndipo mama huyo  alipomshirikisha ‘Engineer’  Jack Ryan  na kazi ikafanyika. Barbara  akapata  mmoja na wengine wakatengenezwa kwa wingi na kuuzwa ulimwengu mzima. Hivyo jina la Barbie lilitokana na jina la mtoto Barbara.

Barbie ndiyo wanasesere wa kwanza kuandaliwa mikakati ya kimasoko ikiwa ni pamoja na kutengenezewa matangazo ya Televisheni. Wameuzwa sana  ambapo inakadiliwa zaidi ya Barbie milioni moja ziliuzwa katika zaidi nchi 150 duniani. Kwa wastani wanasesere watatu aina ya Barbie waliuzwa kila baada ya sekunde moja, kabla watu wengine hawajaanza kutengeneza aina zingine zilizonukuliwa kutoka aina hiyo,  zikiwemo za wale unaowaona kwenye maduka  mbalimbali ya  nguo.

Barbie wakiwa wamevaa mavazi maalum ya sikukuu ya Christmas, wameanza kuuzwa rasmi  Novemba 15, 2013 katika duka jipya la wanasesere lililoko jijini London  Uingereza kwa bei ya  £250 kila moja ambayo ni zaidi ya shilingi 500,000 za kitanzania.

Mbunifu wa mavazi hayo Stephen Jones ambaye ni maarufu  zaidi  kwa utengenezaji wa kofia za wanawake alisema Ruth Handler alikwenda kazini kwake kununua kofia kwa ajili ya sikukuu, lakini matokeo yake ikawa ni kumpata kama mteja mpya, mkubwa na  ambaye  atazidi kuwa nae. Alitengenezewa aina 5 za  nguo zenye mandhali ya ‘Christmas’kwa ajili ya Barbie ambapo kila nguo ilipewa jina lake. “Kilichonihamasisha zaidi kubuni mavazi haya ni utamaduni na mandhali ya sikukuu yenyewe”, alimaliza kuongea Stephen Jones huku akicheka.
 Vazi hili linaitwa 'Christmas Tree Barbie'

 'Toffee Ice Barbie'
'Snow Globe Barbie'
 'Santa Baby Barbie'

 'Glamorous outfits Barbie'
Stephen Jones (Katikati)

Wednesday, November 27, 2013

MAKOSA 5 YA KIMASOKO YANAYOFANYWA NA WASANII KUHUSU MITANDAO YA KIJAMII NA JINSI YA KUYAREKEBISHA

Maoni ya semadat blog


AY, Miongoni mwa wanamuziki wa nchini Tanzania wanaotumia vizuri nafasi ya mitandao ya 
kijamii kujitangaza


1. Kutoingia kabisa: Msanii hasipoingia katika ulimwengu huu wa mitandao ya kijamii anakosa nafasi muhimu ya kujitangaza mwenyewe. Japo wengine husema hawana muda au hawawezi kutumia hii teknolojia, kuna haja ya kuingia japo dakika 30 tu kwa siku ndani ya mitandao hii.

Tafuta mtu wa  kukusaidia ambaye atafanya yote yanayotakiwa kufanyika kila unapohitaji kufanya hivyo. Kama tatizo ni muda, basi afanye hivyo badala yako kwa muda ambao haupo na kama  tatizo ni kutoweza kutumia, awepo muda wote wakati huo ukijifunza taratibu.


2. Kuingia tu pasipo kutumia:  Kuwa kwenye mitandao ya kijamii na kuweka taarifa zako, kwa mfano wewe ni nani, unafanya nini, njia ya kukupata n.k, ni mambo muhimu zaidi, lakini lazima pia kila unaporudi  uwe na sababu.

Hakikisha unakuja na jambo lolote, kama ni taarifa au jambo lolote la kuwafanya watu wajue kinachoendelea kuhusu wewe, wasanii wengine au matukio mbalimbali.


3. Kutofanya kama unavyotaka kufanyiwa: Ukiuliza ni wangapi wanasema asante kwa watu waliowafuata kwenye mitandao yao ya kijamii utapata mmoja kati ya mia moja. Pia ni wachache sana huwafuata wengine badala ya kungoja wafuatwe kwenye Facebook, Twitter au Instagram na mitandao mingine.

Mitandao ya kijamii ni kwa ajili ya mawasiliano na uhusiano, pia ni vyombo ya kujitangaza kwa njia ya mtandao wa intaneti. Ukijenga uhusiano mzuri utawaweka mashabiki wako karibu na wewe zaidi. Pia ni vizuri wakati mwingine kuzungumzia mambo mengine na wasanii wengine tofauti na kazi zako, kuwatangaza wasanii wengine, kuwashauri na kuwakosoa itakuongezea mashabiki wengine kutoka kwao.


4. Kuhama mitandao badala ya kuongeza: Wapo wanaozani mitandao ya kijamii ni fasheni. Kila mtandao una faida zake na mapungufu yake, ndiyo maana kila kukicha inaibuka mingine ili kuziba mapengo lakini haimaanishi kwamba  ndiyo bora zaidi.

Jitaidi kuwa sehemu nyingi kwa kadri inavyowezekana, pia ongeza ufahamu juu ya mitandao hii.Ukifanya hivyo utaelewa umuhimu wa kila mtandao, umaarufu wake na matumizi yake. Husiondoke Facebook kwenda Instagram, badala yake endelea kuwa FB na fungua akaunti ya Instagram pia. Huu ni mfano.


5. Kutofikiria kama ‘Brand’: Hapa namaanisha jina linalofahamika kibiashara au lenye lengo la kufahamika kwa ajili hiyo. Jina la msanii ni kama jina la kampuni, taasisi, mkoa au nchi. Baadhi ya wasanii hutumia mitandao ya kijamii kama mtu yeyote mwenye lengo tu la kujenga mtandao na marafiki zake kwa ajili ya kupashana habari na kuwasiliana kwa ujumbe mfupi wa maneno.

Si vizuri kutumia majina tofauti kwenye mitandao ya kijamii, kama jina lako ni ‘Christmas Day’ na ndilo jina unalotumia Facebook, kwenye Twitter, husitumie ‘Christmas Eve’. Kumbuka kuwa na rangi zako kama ilivyo Bendera ya Taifa, Nembo ya Taifa au ya kampuni, ili zitumike kujenga uhusiano kati ya mitandao ya kijamii unayotumia, picha za kurasa za mwanzo za mitandao hiyo zisiwe na tofauti sana. Pia ni muhimu kuzingatia fursa zinazotolewa na baadhi ya mitandao kutofautisha matumizi ya kawaida na ya kibiashara. Kwa mfano, hata Facebook watashangaa kama unatumia akaunti kujitangaza badala ya kuwa na akaunti alafu ndani yake ukafungua ukurasa maalum kwa ajili  hiyo yaani ‘Facebook Page’.

Wema Sepetu, msanii wa Filamu nchini Tanzania ambaye pia anatumia vizuri fursa ya mitandao ya kijamii

Amanda  Bynes, muigizaji wa nchini Marekani anayetajwa kama miongoni mwa watumiaji wazuri wa mitandao ya kijamii  katika kazi zake za sanaa

 Amanda Bynes

MAGARI MAPYA YENYE TABIA ZA KIFERRARI YALIYOINGIA SOKONI MWAKA HUU

Mjapani Ken Kiyoyuki Okuyama ni  mbunifu wa magari ambaye alishirikiana kwa kiasi kikubwa na muitaliano Ferrari Enzo  katika kufanikisha uwepo wa gari aina ya Ferrari. Pia alikuwa ameajiriwa na kampuni ya Porsche ambapo pia alisaidia katika ubunifu wa gari aina ya Bxster.

Mwaka huu katika maonyesho ya magari ya Tokyo ‘Tokyo Motor Show’ anaonyesha   magari manne aliyoyabuni kama sehemu ya ‘Brand’ yake binafsi ya ‘Ken Okuyama Design’. Matatu ni  kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya usafiri barabarani na moja kwa ajili ya matumizi ya uzalishaji mashambani.



Sunday, November 24, 2013

P-SQUARE WAWASHA MOTO TANZANIA- HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA KATIKA VIWANJA VYA LEADER JIJINI DAR ES SALAAM

Joh Makini
P-Square
Ben Paul

Lady Jaydee

Profesor J
Weusi ( Nick wa pili na G-Nako)
Picha na Global Publishers.info

FAHAMU MAMBO 10 MUHIMU KUHUSU P-SQUARE


Wakati  wanamuziki hawa kutoka Nigeria wakiwa tayari wamefanya kazi yao hapa Dar es salaam, Tanzania, semadat inakuletea mambo kumi yakiwemo unayoyajua na husiyoyajua kuhusu P-SQUARE.
Kaka yao mkubwa Jude Okoye ambaye pia Mtayarishaji wa muziki kupitia 'Square Records Limited'

1.Walianza kujihusisha na muziki  wakiwa shuleni katika shule ya sekondari st Murumba nchini Nigeria ambapo waliimba na kucheza nyimbo za wanamuziki wengine akiwemo M.C. Hummer, Bobby Brown, Michael Jackson na wengine.


2. Baada ya hapo walianzisha kundi la kuimba Acapella, yaani kuimba bila ala yoyote ya muziki wakiwa watu watano ambao ni M Clef , Michael, Melvin, Peter and Paul, kundi lilioitwa “MMMPP”


3. Mwaka 1997, Peter na Paul waliamua kujikita zaidi kwenye fani ya kucheza muziki na kuanzisha kundi lao lililoitwa Smooth Criminals wakimtizama Michael Jackson kama ‘Role model’ wao.


4. Walisoma ‘Business Administration’ katika chuo kikuu cha Abuja


5.  Kabla hawajajiita  P-square walianza na  majina  ‘Double P’ baadae  P&P, likafuatia Da Pees, ndipo likaja P-Square wanalolitumia mpaka sasa.


6. Katika familia yao wana ndugu zao sita (6) ambao ni Ifeanyi, Henry, Jude, Lillian, Tony and Mary.


7. Kaka yao mkubwa Jude ‘Engees’ Okoye ndiye ‘Producer’ au mtayarishaji wa kwanza wa kazi zao za 

muziki kabla hawajaingia kwenye ‘Label’ ya ‘Konvict’ inayomilikiwa na Akon. Ndiye CEO wa Square Records Limited  na  Northside Entertainment Limited ambazo zilishughurika kuwakuza kimuziki na  kuwafikisha walipo sasa na mpaka sasa ndiye msimamizi wa kazi zao za muziki.

8.  Ni miongoni mwa wanamuziki 5 bora kwa utajiri barani Afrika.


9. Wanatumia ndege yao binafsi


10. Wana  nidhamu kubwa ya matumizi ya pesa na wako makini kwa wale wanaowafuata  kwa lengo la “kuchop” pesa  zao.

P-Square wakiwa na Mr MayD, mmoja wa wasanii walioimba nao wimbo uliowatangaza sana kimataifa wa 'Chop my money'

P-SQUARE, VODACOM, EATV/EA-RADIO NA MATUKIO KATIKA PICHA

 P-Square wakiwa Tanzania , kwenye picha ya pamoja  kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha masoko na mawasiliano wa Vodacom  Kelvin Twissa, Paul na Peter,  Mkuu wa East Africa Radio Nasser Kingo na msanii wa Bongo Flava Ben Paul.

Mapacha wa P-Square, kushoto ni Peter Okoye, kulia ni Paul Okoye  na katikati ni Mkuu wa Vodacom Foundation Yessaya Mwakifulefule wakicheza na watoto wa shule maalum ya msingi ya Msimbazi walipotoa msaada wa chakula na mahitaji mengine ya kibinadamu

Friday, November 22, 2013

MR MAY "D" AONYESHA ANAVYOISHI KUPITIA INSTARGRAM


Mr May D

Mwanamuziki aliyekalia 'VERSE' ya mwisho kwenye wimbo wa "CHOP MY MONEY" ambao P-square walimshirikisha yeye na Akon, Mr MayD a.k.a 'Sure Boy' ameandika kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram kwamba "Hivi ndivyo  ninavyoishi", na kuweka picha zinazoonyesha sehemu mbalimbali za ndani ya nyumba yake na nje. Katika picha moja ameonekana akiwa pembeni mwa gari dogo la kifahari.


TUMEKUJA TANZANIA KUTOA BURUDANI YA ZAIDI YA MASAA MAWILI NA YA UHAKIKA-P-SQUARE

P-square baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa ya Mwl Nyerere jijini Dar es Salaam

DAVIDO ASAIDIA WANAFUNZI NA WATOTO YATIMA KATIKA SIKU YAKE YA KUZALIWA

Davido akiwa na mlezi wa watoto yatima


Siku ya jana Novemba 21, 2013,  ni siku ambayo mwanamuziki wa miondoko ya Afro Pop wa nchini Nigeria anayeitwa David, au  maarufu kama ‘Davido ameongeza mwaka mmoja katika umri wake. Ameitumia  siku yake hiyo ya kuzaliwa kuwatembelea na kuwapa msaada wanafunzi na watoto yatima.

Mwanamuziki huyo ambaye anatarajia kuachia wimbo wake mpya hivi karibuni, aliianzia siku yake katika shule ya msingi ya Ikeja ambayo ni ya serikali ambapo alitoa vifaa vya kufundishia na vifaa vya masomo kwa ajili ya wanafunzi. Baada ya hapo alielekea kwenye vituo cha watoto yatima vya ‘Heart of Gold Children's Hospice’ na  ‘Heritage Homes Orphanage’ ambako alitoa zawadi mbali mbali. Mtandao wa lindaikeji uliandika.

ALBAM MPYA YA MALKIA WA TWITTER INAYOITWA 'ARTPOP' YASHIKA NAMBA MOJA CHART ZA BILLBOARD

Lady Gaga

Albam mpya ya mwanamuziki Lady Gaga a.k.a Malkia wa Twitter ambayo inaitwa 'ARTPOP',iko nafasi ya juu kabisa kwenye chart za Billboard wiki hii baada ya kuuza nakala 258,000 wiki ya kwanza. Ni albam yake ya tano kuingia kumi bora ya chart hizo 'baada ya 'Born This Way', 'The Fame', 'The Fame Monster' na 'The Remix'. Artpop ya Lady Gaga ni albam ya tatu ya mwanamuziki wa kike kuchukua nafasi hiyo mwaka huu, baada  'Prism' ya Katy Perry ambayo iliuza nakala 286,000 na 'Bangerz' ya Miley Cyrus iliyouza nakala 270,000 .

Moja ya mbwembwe za kuitangaza albam yake

Hata hivyo Lady Gaga amesikitishwa na yanayozungumzwa na watu, wakiwemo mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii na yanayozungumzwa na vyombo vya habari. Kwa ufupi amesema watu wanamchukia. Inasemekana wengi hawakufurahishwa na jinsi alivyofanya onyesho la 'Saturday Night Live'  wikend iliyopita ambapo alipitiliza na kuonyesha vitendo vya aibu alipokuwa akicheza wimbo wa 'Do what you want' na R. Kelly ambao umo kwenye hiyo albam yake mpya na aliomshirikisha gwiji huyo wa muziki wa RnB.
 Lady Gaga na R. Kelly wakifanya onyesho la wimbo wa 'Do what you want' 


Lady Gaga aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba ana mapenzi makubwa na muziki na yote anafanya kwa ajili ya mashabiki wake, anashindwa kuelewa chuki zinazomkabili. "Labda ndivyo burudani ya sasa ilivyo, watu wanafurahia zaidi kumnyooshea mtu kidole na kumcheka zaidi ya kumsifia kwa mazuri anayofanya, nitaendelea kufanya mazoezi na kujaribu", alimalizia kuandika kwenye Twitter siku ya Jumanne Novemba 20, 2013.
Alichoandika kwenye Twitter 

 Lady Gaga anajulikana kama Malkia wa Twitter tangu alipokuwa mtu wa kwanza duniani kufikisha idadi ya wafuasi (Followes) milioni 20 kwenye Twitter,  Machi 2012 na kupewa taji hilo. Aliingia kwenye mtandao huo Machi 26, 2008. Nyimbo zilizomo kwenye albam yake hiyo ni:

1.    Aura
2.    Venus
3.    G.U.Y. (Girl Under You)
4.    Sexxx Dreams
5.    Jewels & Drugs (featuring T.I., Too $hort & Twista) [Explicit]
6.    MANICURE
7.    Do What You Want (featuring R. Kelly) [Explicit]
8.    ARTPOP
9.    Swine
10.   Donatella
11.   Fashion!
12.   Mary Jane Holland
13.   Dope
14.   Gypsy
15.   Applause