UA-45153891-1

Thursday, November 14, 2013

HARUSI YA 'PETER WA P-SQUARE' NA 'LOLA OMOTAYO' YANUKIA


 Peter na Lola

Siku ya jumapili Novemba 17, 2013 ikiwa ni siku tano tu kabla ya mapacha wa kundi la P-Square kufanya onyesho jijini Dar es salaam, familia ya Bwana Okoye ambaye ni baba wa vijana hao itakuwa na tukio la kihistoria la harusi ya kiutamaduni kati ya mmoja wa mapacha hao anayeitwa Peter Okoye na mpenzi wake wa muda mrefu Lola Omutayo ambaye alivishwa pete ya uchumba siku kadhaa zilizopita.

Kamati ya maandalizi ya harusi hiyo imesema kadi ya mialiko ambazo zimetengenezwa kwa ‘chip’ ya ki-electroniki zimeshatumwa karibu kwa wageni wote wanaotarajiwa kushuhudia tukio hilo, na bado zingine zinawasubiri watu wengi maarufu watakaotoka nje ya nchi ambao hawakutajwa.
 Kadi ya Harusi ya Peter na Lola itakayofanyika Jumapili Novemba 17, 2013

Lola Omutayo ambaye  alikuwa na ndoto za kuwa msanii wa Nollywood, siku za nyuma alienda nchini Marekani  kusoma ambapo alipata shahada ya  “Theatre Arts”  kutoka chuo kikuu cha Francisco. Aliporudi nchini Nigeria aliajiriwa na kampuni ya ECONET  ambayo kwa sasa ni  Airtel kama Meneja matukio na baadae kuhamia kampuni ya matangazo ya Daily Times na kisha kwenye kampuni ya mafuta na gesi inayomilikiwa na baba yake.

 Anasema alikutana na Peter kikazi wakati kampuni ya British American Tobacco (BAT) ambayo ni moja ya wateja wa kampuni ya baba yake ilipokuwa ikifanya shughuri za kimatangazo na P-Square, ndivyo alivyokutana  na Peter. Lola na Peter  wana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Cameron.

Peter na Lola kwenye 'Birthday' ya mtoto wao

Ingawa mama mzazi wa Peter alishatangulia mbele ya haki, mwaka mmoja uliopita, baba yake atawaongoza wanae na ndugu wa karibu wa familia kutoka kijiji cha Akwa jimboni Anambra kwenda Lagos kushuhudia harusi hiyo. Peter mwenye umri wa miaka 33 anakuwa mtoto wa kwanza wa Mzee Okoye kuoa. Pacha wake Paul bado hajaoa lakini tayari ametangaza ndoa kwa mpenzi wake anayeitwa Anita Itokwu-Isama. Kaka yao Jude mwenye miaka 38 bado hajamtambulisha yeyote katika familia kama mtarajiwa wake.

No comments:

Post a Comment