UA-45153891-1

Friday, November 22, 2013

ALBAM MPYA YA MALKIA WA TWITTER INAYOITWA 'ARTPOP' YASHIKA NAMBA MOJA CHART ZA BILLBOARD

Lady Gaga

Albam mpya ya mwanamuziki Lady Gaga a.k.a Malkia wa Twitter ambayo inaitwa 'ARTPOP',iko nafasi ya juu kabisa kwenye chart za Billboard wiki hii baada ya kuuza nakala 258,000 wiki ya kwanza. Ni albam yake ya tano kuingia kumi bora ya chart hizo 'baada ya 'Born This Way', 'The Fame', 'The Fame Monster' na 'The Remix'. Artpop ya Lady Gaga ni albam ya tatu ya mwanamuziki wa kike kuchukua nafasi hiyo mwaka huu, baada  'Prism' ya Katy Perry ambayo iliuza nakala 286,000 na 'Bangerz' ya Miley Cyrus iliyouza nakala 270,000 .

Moja ya mbwembwe za kuitangaza albam yake

Hata hivyo Lady Gaga amesikitishwa na yanayozungumzwa na watu, wakiwemo mashabiki wake kupitia mitandao ya kijamii na yanayozungumzwa na vyombo vya habari. Kwa ufupi amesema watu wanamchukia. Inasemekana wengi hawakufurahishwa na jinsi alivyofanya onyesho la 'Saturday Night Live'  wikend iliyopita ambapo alipitiliza na kuonyesha vitendo vya aibu alipokuwa akicheza wimbo wa 'Do what you want' na R. Kelly ambao umo kwenye hiyo albam yake mpya na aliomshirikisha gwiji huyo wa muziki wa RnB.
 Lady Gaga na R. Kelly wakifanya onyesho la wimbo wa 'Do what you want' 


Lady Gaga aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kwamba ana mapenzi makubwa na muziki na yote anafanya kwa ajili ya mashabiki wake, anashindwa kuelewa chuki zinazomkabili. "Labda ndivyo burudani ya sasa ilivyo, watu wanafurahia zaidi kumnyooshea mtu kidole na kumcheka zaidi ya kumsifia kwa mazuri anayofanya, nitaendelea kufanya mazoezi na kujaribu", alimalizia kuandika kwenye Twitter siku ya Jumanne Novemba 20, 2013.
Alichoandika kwenye Twitter 

 Lady Gaga anajulikana kama Malkia wa Twitter tangu alipokuwa mtu wa kwanza duniani kufikisha idadi ya wafuasi (Followes) milioni 20 kwenye Twitter,  Machi 2012 na kupewa taji hilo. Aliingia kwenye mtandao huo Machi 26, 2008. Nyimbo zilizomo kwenye albam yake hiyo ni:

1.    Aura
2.    Venus
3.    G.U.Y. (Girl Under You)
4.    Sexxx Dreams
5.    Jewels & Drugs (featuring T.I., Too $hort & Twista) [Explicit]
6.    MANICURE
7.    Do What You Want (featuring R. Kelly) [Explicit]
8.    ARTPOP
9.    Swine
10.   Donatella
11.   Fashion!
12.   Mary Jane Holland
13.   Dope
14.   Gypsy
15.   Applause

No comments:

Post a Comment