Wakati wanamuziki hawa kutoka Nigeria wakiwa tayari wamefanya kazi yao hapa Dar es salaam, Tanzania, semadat inakuletea mambo kumi yakiwemo unayoyajua na husiyoyajua kuhusu P-SQUARE.
Kaka yao mkubwa Jude Okoye ambaye pia Mtayarishaji wa muziki kupitia 'Square Records Limited'
1.Walianza kujihusisha na muziki wakiwa shuleni katika shule ya sekondari st Murumba nchini Nigeria ambapo waliimba na kucheza nyimbo za wanamuziki wengine akiwemo M.C. Hummer, Bobby Brown, Michael Jackson na wengine.
2. Baada ya hapo walianzisha kundi la kuimba Acapella, yaani kuimba bila ala yoyote ya muziki wakiwa watu watano ambao ni M Clef , Michael, Melvin, Peter and Paul, kundi lilioitwa “MMMPP”
3. Mwaka 1997, Peter na Paul waliamua kujikita zaidi kwenye fani ya kucheza muziki na kuanzisha kundi lao lililoitwa Smooth Criminals wakimtizama Michael Jackson kama ‘Role model’ wao.
4. Walisoma ‘Business Administration’ katika chuo kikuu cha Abuja
5. Kabla hawajajiita P-square walianza na majina ‘Double P’ baadae P&P, likafuatia Da Pees, ndipo likaja P-Square wanalolitumia mpaka sasa.
6. Katika familia yao wana ndugu zao sita (6) ambao ni Ifeanyi, Henry, Jude, Lillian, Tony and Mary.
7. Kaka yao mkubwa Jude ‘Engees’ Okoye ndiye ‘Producer’ au mtayarishaji wa kwanza wa kazi zao za
muziki kabla hawajaingia kwenye ‘Label’ ya ‘Konvict’ inayomilikiwa na Akon. Ndiye CEO wa Square Records Limited na Northside Entertainment Limited ambazo zilishughurika kuwakuza kimuziki na kuwafikisha walipo sasa na mpaka sasa ndiye msimamizi wa kazi zao za muziki.
8. Ni miongoni mwa wanamuziki 5 bora kwa utajiri barani Afrika.
9. Wanatumia ndege yao binafsi
10. Wana nidhamu kubwa ya matumizi ya pesa na wako makini kwa wale wanaowafuata kwa lengo la “kuchop” pesa zao.
P-Square wakiwa na Mr MayD, mmoja wa wasanii walioimba nao wimbo uliowatangaza sana kimataifa wa 'Chop my money'
No comments:
Post a Comment