UA-45153891-1

Friday, November 29, 2013

MBUNIFU STEPHEN JONES ATENGENEZA NGUO ZA 'CHRISTMAS' KWA AJILI YA WANASESERE AINA YA BARBIE

Mwanasesere aina ya Barbie

Wakati wabunifu mbalimbali wa mavazi ulimwenguni wakiendelea kuleta mitindo mipya katika tasnia hiyo, mbunifu wa mavazi ya wanawake Stephen Jones ambaye ni muingereza anayefanyia shughuri zake jijini London, amekuza soko lake kwa kuanza kutengeneza mavazi ya wanasesere  ambao kwa  lugha ya kiingereza  wanaitwa ‘Dolls’. 

Kwa kuwa kuna aina zaidi ya moja katika maumbo ya wanasesere, Stephen amechagua kutengeneza mavazi ya wanasesere aina ya Barbie. Ametoa toleo lake la kwanza la mavazi maalum kwa ajili ya msimu wa sikukuu ya ‘Christmas’ ya mwaka huu 2013.


Barbie ni mwanasesere mwenye umbo kubwa  aliyebuniwa mwaka 1959 na mfanyabiashara mwanamke wa kimarekani anayeitwa Ruth Handler . Ilitokea baada ya kumuona mtoto wake wa kike  anayeitwa Barbara akitamani mwanasesere aliyekuwa nae awe mkubwa  kama  mtoto  wa zaidi ya miaka mitano badala ya kumuona  siku zote akiwa kama mtoto mchanga. Ndipo mama huyo  alipomshirikisha ‘Engineer’  Jack Ryan  na kazi ikafanyika. Barbara  akapata  mmoja na wengine wakatengenezwa kwa wingi na kuuzwa ulimwengu mzima. Hivyo jina la Barbie lilitokana na jina la mtoto Barbara.

Barbie ndiyo wanasesere wa kwanza kuandaliwa mikakati ya kimasoko ikiwa ni pamoja na kutengenezewa matangazo ya Televisheni. Wameuzwa sana  ambapo inakadiliwa zaidi ya Barbie milioni moja ziliuzwa katika zaidi nchi 150 duniani. Kwa wastani wanasesere watatu aina ya Barbie waliuzwa kila baada ya sekunde moja, kabla watu wengine hawajaanza kutengeneza aina zingine zilizonukuliwa kutoka aina hiyo,  zikiwemo za wale unaowaona kwenye maduka  mbalimbali ya  nguo.

Barbie wakiwa wamevaa mavazi maalum ya sikukuu ya Christmas, wameanza kuuzwa rasmi  Novemba 15, 2013 katika duka jipya la wanasesere lililoko jijini London  Uingereza kwa bei ya  £250 kila moja ambayo ni zaidi ya shilingi 500,000 za kitanzania.

Mbunifu wa mavazi hayo Stephen Jones ambaye ni maarufu  zaidi  kwa utengenezaji wa kofia za wanawake alisema Ruth Handler alikwenda kazini kwake kununua kofia kwa ajili ya sikukuu, lakini matokeo yake ikawa ni kumpata kama mteja mpya, mkubwa na  ambaye  atazidi kuwa nae. Alitengenezewa aina 5 za  nguo zenye mandhali ya ‘Christmas’kwa ajili ya Barbie ambapo kila nguo ilipewa jina lake. “Kilichonihamasisha zaidi kubuni mavazi haya ni utamaduni na mandhali ya sikukuu yenyewe”, alimaliza kuongea Stephen Jones huku akicheka.
 Vazi hili linaitwa 'Christmas Tree Barbie'

 'Toffee Ice Barbie'
'Snow Globe Barbie'
 'Santa Baby Barbie'

 'Glamorous outfits Barbie'
Stephen Jones (Katikati)

No comments:

Post a Comment