Mke wa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Asha Bilal
Mke wa Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bi Asha Bilal, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maonyesho ya mitindo ya kimataifa ya mavazi ya kanga, yanayojulikana kama ‘Kanga za Kale.
Maonyesho hayo yatafanyika katika Hoteli ya Serena ijumaa wiki hii, yatakusanya watu wengi maarufu ambapo mke huyo wa makamu wa Rais atawaongoza mashabiki wa fani ya mitindo ya mavazi akiwa katika vazi la Kanga.
Mkurugenzi wa Fabak Fashion, Asia Idarous, ambao ndio waandaji wa maonyesho hayo, amesema tofauti na maonyesho mengine yaliyotangulia, Kanga ya Kale ya mwaka huu ina ladha tofauti kidogo.
“Licha ya kuonyesha matoleo mapya na mitindo ya kanga pia kuonyesha yale ya zamani ili kuleta vionjo zaidi kwa wavaaji wa sasa, tunakusudia kutoa darasa kuhusiana na thamani ya kanga japo kwa muda mfupi tu”, anasema.
Watakaofika kwenye maonyesho pia watapata burudani kutoka katika Kundi la Mashauzi Classic, huku wakishuhudia mitindo kadha wa kadha ya kanga kutoka kwa wabunifu mbalimbali nchini.
Maonyesho ya Kanga za kale nchini yanafanyika kwa mara ya tano tangu pale yalipoanzishwa rasmi mwake mwaka 2008.

Habari:www.mwananchi.co.tz
No comments:
Post a Comment