Kim Kardashian akiwa na Kanye West
Alipokuwa tayari anafuatwa na watu 5,731,011 kwenye Instagram, mwanamuziki Kim Kardashian alitangaza kujitoa kwenye mtandao huo kwa kufunga akaunti yake mwishoni mwa mwaka jana. Ni baada ya Instagram kuongeza kipengere cha vigezo na masharti ya kutumia mtandao huo Desemba 17, 2012 ambacho kingepelekea picha za watumiaji kuuzwa kwa ajiri ya matangazo pasipokuwalipa wamiliki wa picha hizo.
Maelezo yalikuwa kama ifuatavyo “Unakubari kwamba kampuni au biashara yoyote inaweza kutulipa kuonyesha picha zako, jina lako na mambo mengine kwa ajiri ya matangazo nawewe husipate malipo yoyote”.
Hata hivyo, siku moja baada ya hapo, Instagram iliwaomba radhi watumiaji wake kwa kusema kwamba, lengo lao lilikuwa kufanya majaribio ya tekinolojia ya matangazo ya mtandao huo japo maelezo yao hawakuyaweka vizuri na watumiaji wakaelewa visivyo.
Kujitoa kwa Kim Kardashian ambaye ndiye alikuwa anaongoza kwa kuwa na wafuasi wengi akifuatiwa na Justin Bieber aliyekuwa na wafuasi milioni 4.3 na Obama wafuasi milioni 1.8, kungepelekea kujitoa kwa ndugu zake Khloe, Kylie, Kendall na Rob Kardashian ambao wote walikuwa katika kumi bora ya waliofuatwa na watu wengi kwenye mtandao huo kwa wakati huo.
Kim Kardashian aliendelea kubaki Instagram na mpaka kufikia mwishoni mwa September 2013 alikuwa akifuatwa na watu 9, 935, 306. Ni wa 3 kati ya akaunti 10 duniani zilizofuatwa na watu wengi kwenye mtandao huo akiwa tayari amepitwa na Justin Bieber mwenye watu 10,822, 685 ambaye anachukua namba 2 akitanguliwa na Instagram yenyewe ambayo ndiyo namba 1 .
Inasemekana ujauzito wake na kujifungua vimechangia Kim kupitwa na Justin Bieber kutokana na kuwa muda mrefu mbali na Kamera na picha zake kutosambaa zaidi ikilinganishwa na awali. Kim Kardashian ni mama wa mototo wa Kanye West.