UA-45153891-1

Monday, September 30, 2013

VANESSA MDEE- MWANASHERIA ANAYETUMIA VIPAJI VYAKE IPASAVYO




Vanessa  Mdee  alizaliwa Tanzania mwaka 1988 na kukulia New York, Paris, Nairobi na Arusha.

Japo alisoma sheria ‘Catholic  University of Eastern Africa’ ,ubunifu kupitia sanaa ndicho kitu ambacho kilikuwa tayari kiko kwenye damu yake. Tangu aliposhinda kwenye VJ search hapa nchini Tanzania mwaka 2007, vipaji vyake vingi vilizidi kuibuka na kumfanya asonge mbele zaidi.  Akiwa na umri wa miaka 19 tu Vanessa aliondoka nchini akiwa mtanzania wa kwanza kufanya kazi MTV akiungana na waendeshaji (VJs) wengine kwenye kipindi cha Coca Cola Chart.

Mwaka mmoja baada ya hapo Vanessa alifahamika sana kwenye sekta ya burudani Tanzania na bara zima la Afrika kwa kushiriki maonyesho mbalimbali nchini Nigeria, Afrika kusini, Kenya, Msumbiji, Angola, Uganda, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Tanzania, Marekani na  Brazil.


Mwaka 2008 Vanessa alifanya kazi na “MTV Staying Alive Foundation” akishughurika na mambo mbalimbali za kijamii hasa yanayohusu vijana ambao wanataka kubadilika na kuleta mabadiliko kwenye jamii zao kupitia kazi za ubunifu ikiwa pamoja na muziki. Mwanzoni mwa mwaka 2009 alitangaza kwenye onyesho la “Senses, Sounds and Wisdom” katika tamasha la kimataifa la muziki  la Sauti Za Busara ambapo pia aliweza kujitambulisha kiutamaduni na mambo ya mitindo kupitia ‘Swahili Culture’ na ‘Vee-style’

Shughuri za mitindo zikamfanya awe mtangazaji kwenye matukio ya MAMA (MTV AFRICA MUSIC AWARD) kwa miaka 3 mfululizo, kabla hajawa mtangazaji wa redio Choice FM ya hapa nchini Tanzania. Ni mwanaharakati wa mapambano dhidi ya Ukimwi na mwakilishi wa UNAIDS, akihusika na habari juu ya janga hilo kupitia MTV na tovuti (website) yake.

Pia ni mwanamuziki ambaye anafanya vizuri kupitia nyimbo zake na zile alizoshirikishwa na wanamuziki wengine wa hapa nchini Tanzania.

 
Vanessa Hau Mdee, a.k.a. Vee akiwa studio na Ludacris

MICHUZI-FAMILIA YA ‘BLOGGERS’ NCHINI TANZANIA

Muhidin Issa Michuzi akizungumza jambo kwenye moja ya makongamano
                              

UKITEMBELEA mtandaoni utakutana na  neno  'Michuzi' kwa majina mengine tofauti na Issa Michuzi mmiliki wa Michuzi Blog. Ni Blogs au maarufu kama Blogu zinazomilikiwa na watanzania wengine wanaotokea katika familia moja na Blogger huyo mkongwe Muhidin Issa Michuzi.

Safari yake ilianza kwa kupenda kazi ya kupiga picha na kusomea fani hiyo miaka ya 80. Akiwa anaendelea na shuguri zake, siku flani  moja ya picha zake ikachaguliwa kuingia kwenye ukurasa wa mbele wa  gazeti la serikali la Daily News , akaendelea  kufanya kazi na gazeti hilo na kisha kuajiriwa kabisa na chombo hicho cha habari mwanzoni mwa mwaka 1990. Baadae aliongeza taaluma ya ‘Photojournalism’ mjini Berlin na  uandishi wa habari  Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kumaliza mwaka 1996.

Alianza kazi ya Blogu  mwaka 2005 ambapo kwa mara ya kwanza Blogu yake iliingia mtandaoni Septemba 8, 2005. Lengo lake kuu ikiwa ni kuwapa watu habari zinazohusu nchi ya Tanzania kupitia Blogu ya picha “photoblog.

Mpaka sasa anamiliki tuzo nyingi ikiwa ni pamoja na Blogu inayoongoza Tanzania kutoka ‘1st Annual Tanzanian Blog Awards’,  Blogu bora ya habari za siasa mwaka 2011 kutoka ‘VADE Local Digital Media’ na ‘Vodacom Awards for Digital Excellence’ mwaka 2012.

Ndugu zake ambao pia wanafahamika kama Bloggers ni Ahmad and Othman na pamoja wameanzisha kampuni ya habari ambayo inaitwa Michuzi Media Group (MMG).
.

Saturday, September 28, 2013

MISS PHILIPPINES MEGAN YOUNG ACHUKUA TAJI LA MISS WORLD 2013


 MISS WORLD 2013-Megan Young wa Philipines

Megan Young wa Philipines ndiye aliyenyakua taji la shindano la Miss World 2013, lililofanyika Bali Indonesia leo Septemba 28, 2013.

Ameandika kwenya ukurasa wake wa facebook kwamba aliteleza na kuanguka kabla hajapanda stejini kwenye shindano la Top Modal.  Aliongeza kwamba hakutegemea angeshinda kutokana  na kwamba si mrefu akijilinganisha na washiriki wengine walivyokuwa.” Kwa kufikiria hilo la kutokuwa mrefu, imenifanya niongeze juhudi zaidi kuutafuta ushindi”.Ameandika  Megan Young, Miss World 2013.

Shindano limemalizika huku Miss Brazil Sancler Frantz akichukua tuzo ya Miss Beach Beauty, Miss Netherlands Jacqueline Steenbeek akichukua tuzo ya  Miss Sportswoman, Miss India Navneet Kaur akiondoka na tuzo ya Miss Multimedia  pamoja na  Miss Nepal Ishani Shrestha kunyakua tuzo ya Miss Beauty with a Purpose.

                     Miss Brazil Sancler Frantz aliyechukua 'Miss Beach Beauty Award'
Miss Netherlands Jacqueline Steenbeek aliyechukua ' Miss Sportswoman Award
 Miss India Navneet Kaur aliyechukua  Miss Multimedia Award
Miss Nepal Ishani aliyechukua Miss Beauty with a Purpose Award
 Washiriki wakati wa shindano la Miss Word 2013 leo Sept 28,2013

Friday, September 27, 2013

FAHAMU MASHINDANO 5 YA UREMBO YENYE UMAARUFU MKUBWA DUNIANI

WAKATI wadau, wapenzi na mashabiki  wa  Urembo na Mitindo ulimwenguni wakingoja nani atatangazwa mshindi wa Miss World 2013 na atatoka nchi gani kesho Septemba 28, fahamu mashindano 5 ya urembo yanayoongoza kwa kufahamika zaidi Ulimwenguni.

1. MISS WORLD

Hili ndilo shindano kubwa kuliko yote ulimwenguni lilianzishwa mwaka 1951 nchini Uingereza na mjasiliamali Erick Morley akiwa na mke wake Julia Morley. Ndilo shindano lenye umaarufu kushinda yote na linalotangazwa na vyombo ya habari vingi ulimwenguni. Kwa mwaka huu litafanyika Septemba 28 jijni Bali, nchini Indonesia. Nchi ya Tanzania inawakilishwa na Brigitte Alfred.
                                                Miss Tanzanai 2012- Brigitte Alfred.

    
  2. MISS UNIVERSE
 
Hili ndilo shindano linalofuatia baada ya MissWord. Lilianzishwa mwaka 1952 nchini Marekani na kampuni ya mavazi ya Pacific Mills jimboni Calfornia kabla ya kumilikiwa na Donard Trump. Lilibadilishwa jina kutoka Miss Universe Inc na kuitwa Miss Universe Organization mwaka 1998 na makao yake makuu yakaamishwa kutoka  Los Angeles, California, kwenda New York . Kwa hapa Tanzania, aliyeshinda mwaka jana (2012) kushiriki mashindano hayo ni Winfrida Dominic.
 Miss Universe Tanzania 2012-Winfrida Dominic.

    3. MISS INTERNATIONAL
Ni shindano la urembo lililoanzishwa nchini Marekani mwaka 1960 jimboni California na kuhamishiwa jijini Tokyo nchini Marekani ambako ndiyo makao makuu yake.Mwaka 2011, Tanzania iliwakilishwa na mrembo Nelly Kamwelu ambaye pia kwa mwaka huo huo alishiriki mashindano matatu kuiwakilisha Tanzania, ambayo ni Miss Universe Tanzania ,Miss Southern Africa International na  Miss International 2011.

 Miss International Tanzania-Nelly Kamwelu

4. MISS EARTH
4.   Ni miongoni mwa mashindano makubwa manne ya urembo duniani. Lianzishwa mwaka 2001 na liko chini ya Miss Earth Foundation. Lilianzishwa kwa ajiri ya kuhamasisha utunzaji wa mazingira na mshindi wa shindano hilo ndiye msemaji wa Miss Earth Foundation na shirika la uratibu wa shughuri za mazingira la umoja wa mataifaHYPERLINK "http://en.wikipedia.org/wiki/United_Nations_Envi(UNEP) na mashirika mengine ya mazingira. Aliyeshinda mwaka 2012 kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo ni Bahati Chando.
    Miss Earth Tanzania 2012- Bahati Chando.

        5. MISS TOURISM (MISS UTALII)
Ni miongoni mwa mashindano maarufu ya urembo ulimwenguni, Kwa mara ya kwanza Tanzania ilifanya vizuri katika shindano hilo ambapo mshiriki Nelly Kamwelu ambaye alikuwa mshindi wa 5.  Aliyeshinda  mwaka 2012 kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo ni Hadija Saidi Mswaga.
 Miss Tourism Tanzania 2012/2013-Hadija Saidi Mswaga.

Thursday, September 26, 2013

PETER MSECHU AWAFUTA MACHOZI WANANCHI WA KENYA


Peter Msechu

Msanii wa Bongo Flava Peter Msechu, ametunga na kurekodi wimbo unaoitwa KENYA TUTADUMU, kwa ajiri ya kuwafariji wanananchi wa Kenya kufuatia tukio la ugaidi lililofanyika nchini humo katika jengo la biashara la Westgate. Amesema nchi ya Kenya ina mchango mkubwa kwake yeye mpaka alipofikia na ameguswa sana hasa ikizingatiwa kwamba Kenya ni nchi na iko kwenye muungano wa Afrika Mashariki sawa na nchi yake ya Tanzania.

GORAN TOMASEVIC, MPIGA PICHA WA KIMATAIFA NA MWANDISHI WA HABARI ZA KIVITA ALIVYOFANYA KAZI KWENYE TUKIO LA ‘WESTGATE MALL’ NCHINI KENYA

Jengo la Westgate likiwa tayari limetekwa

Kama umekuwa ukifuatilia tukio la kigaidi la nchini Kenya kufuatia uvamizi na utekaji wa Jengo la 'Westgate Mall' utakuwa umekutana na picha za kipekee (exclusive photos) zilizochukuliwa ndani ya jengo hilo wakati uokoaji ukiendelea. Aliyekuwa akifanya yote hayo nyuma ya Kamera si mwingine bali Goran Tomasevic. Ni mwandishi wa habari upande wa upigaji wa picha ambaye ni mkongwe mwenye uzoefu wa miaka 20. Anashughurika na matukio ya hatari hasa yale ya kivita. Kwa muda huo amekuwa mpiga picha kwenye migogoro mbalimbali ikiwemo ya Afghanistan, Iraq, Libya, Misri na Syria. Kwa sasa anafanyia kazi nchini Kenya.

Mpiga picha Goran Tomasevic

Ifuatayo ni stori  fupi aliyoitoa kuhusu tukio la Westgate," Nilikuwa nyumbani niliposikia kutoka kwa rafiki yangu mmoja kwamba kuna jambo limetokea japo wote hatukuwa na uhakika ni kitu gani, Tulienda mpaka maeneo ya jengo la Wastage Mall na kuona baadhi ya miili imelala maeneo ya kuegesha magari, basi hapo nikagundua hili si jambo la kawaida.  Niliona baadhi ya askali wa Kenya wakiwa wamejificha pembeni mwa magari nami nikafanya hivyo, huku nikisogelea mlango wa kuingilia, kisha nikaona askali wengine wengi na kuwauliza ni muda gani wataingia ndani, wakaniambia muda huo huo wanaigia ndani ya jengo kupitia juu. Nami nikaigia nao ndani ili kuchukua picha. Pia niliwasaidia askali kwenye baadhi ya matukio ya kuwakomboa mateka".
Zifuatazo ni baadhi ya picha alizopiga nje na ndani ya jengo hilo.



Wednesday, September 25, 2013

MWANAMUZIKI WA KENYA ANNETTE KAWIRA ALIVYOPONEA CHUPUCHUPU KWENYE TUKIO LA UGAIDI LA 'WESTGATE MALL'

                                                               Annette Kawira

MWANAMUZIKI  chipukizi wa nchini Kenya Annette Kawira ambaye anaendelea kupata umaarufu kutokana na wimbo alioshirikishwa na Nonini ambao unaitwa Pole pole, ni miongoni mwa waliokuwa kwenye jengo la biashara la Westgate nchini Kenya wakati likivamiwa na kutekwa na Alshabab.

Ni muda mfupi tu mama yake alikuwa amefika nyumbani akitokea hapa nchini Tanzania. Alimsalimia mama yake kwa furaha na  kumwambia wataongea mengi baadae maana alikuwa tayari amechelewa kazini. Alijiandaa,  akamuaga mama yake, akumbusu mdogo wake wa kiume, kisha akaanza safari kuelekea 'Westgate Mall'.

Anasema alipokuwa ndani ya jengo hilo, akasikia risasi ya kwanza na kuzani ni Transfoma, jambo lililofuata ni kuona mtu mmoja amedondoka chini na damu nyigi zikimtoka. Alianza kuwaza mengi juu ya familia yake na hasa mama yake ambaye akupata hata nafasi ya kuongea nae kabla hajaondoka. Milio ya risasi ilipozidi kuongezeka akaona ndiyo mwisho wake huku akiwaza ni kitu gani kitaandikwa juu ya kumbukumbu yake.

Annette hakupata madhara yoyote isipokuwa mtu mmoja ambaye anafanya nae kazi.Anamshukuru Mungu kwa kumuepusha na anawaombea wote ambao bado wako katika hali ngumu wapate kukombolewa.

Tuesday, September 24, 2013

TAMASHA LA KWANZA LA FILAMU NCHINI TANZANIA KUANZA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Vincent Kigos-RAY 


MTAYARISHAJI na muongozaji Bora wa filamu Swahilihood Vincent Kigosi ‘ Ray the Greatest’ ndiye“Nimefurahia sana kuchaguliwa kuwa ni 'Official Producer' na 'Director' wa tamasha kubwa la filamu linalojulikana kwa jina la Dar Filamu Festival (DFF 2013) lililoanza leo  tarehe 24 na ambalo litamalizika 26 September 2013,katika viwanja vya CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, katika kuhamasisha wapenzi wa filamu kutazama filamu za nyumbani.
   
Tamasha hilo limeandaliwa na kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu wa Filamucentral, ambalo lina lengo la kutoa hamasa kwa jamii kuangalia filamu za Kiswahili.Mratibu wa tamasha hilo, Staford Kihore, alisema kuwa, kwa kuzingatia maendeleo ya filamu siku tatu za tamasha hilo, kila moja imepewa jina, ambako Septemba 24 ni siku ya Bongo Movie Classics, Septemba 25 ni‘Quality Nights’ na siku ya mwisho itakuwa ni ‘Stars Nights’.Alisema, tamasha hilo litapambwa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na Vicent Kigosi ‘Ray’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’.Aliongeza kuwa, tamasha hilo litahusisha filamu za Tanzania pekee na miaka ijayo watashirikisha kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia lugha ya Kiswahili.

Naye Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Geofrey Mahendeka alisema, Septemba 26 ni siku muhimu, kwani taasisi kama Mamlaka ya Mapato (TRA), Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania, Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), na nyinginezo za usambazaji wa filamu zitakuwepo.

Kwa upande wake, Balozi wa Tamasha hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amewaomba watanzania kuliunga mkono tamasha hilo na kuhakikisha linakuwa chachu ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini.Aliongeza kuwa, tamasha hilo litawakutanisha wasanii wote wa filamu na ni jukwaa litakalojenga, kutangaza na kuboresha tasnia ya filamu inayokua kila siku.Tamasha hilo litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu, ambako masomo ya uandishi wa muswada, uigizaji na uongozaji wa filamu yatafundishwa.

Monday, September 23, 2013

LEO DUNIANI: TAMASHA LA MWISHO LA BOB MARLEY



SIKU ya leo, wanamuziki wa Reggae, mashabiki wa muziki huo na wapenzi wa muziki kwa ujumla, wanaikumbuka siku ya mwisho kufanya tamasha la muziki ya gwiji wa miondoko hiyo hayati Bob Marley. Tarehe ya Septemba 23, 1980, Bob Marley alifanya tamasha la mwisho 'Bob Marley's last ever concert'ndani ya Stanley Theatre, Pittsburgh kabla hajarudi nyumbani Jamaica kumalizia muda wake wa mwisho baada ya matibabu ya maradhi ya saratani yaliyokuwa yakimsumbua kutofanikiwa.

Alifariki dunia Mei 11, 1981 akiwa na umri wa miaka 36 na maneno ya mwisho aliyaongea kwa mtoto wake Ziggy akisema ‘Money can’t buy life.’yaani pesa haiwezi kununua maisha. Albam yake ya 'Exodus'ilitajwa na jarida la 'Times' kama albam bora ya karne ya 20. Kwa muda mfupi alioishi duniani, alitambulika ulimwengu mzima na muziki wake ukabaki kama alama ya maisha yake na kipaji chake.

Sunday, September 22, 2013

MISS TANZANIA 2013 KUFUATA NYAYO ZA NANCY SUMARI

Redd’s Miss Tanzania 2013 , Happiness Watimanywa, mshindi wa pili Latifa Mohamed (kushoto) na wa tatu ni Clara Bayo ambapo jumla ya Warembo 30 walishiriki kutoka mikoa ya Tanzania.
 Gari alilozawadiwa
 
Tano bora ya washiriki
Kumi bora ya washiriki
Miss Tanzania 2013 akiwa na washiriki wenzake

Saturday, September 21, 2013

"TATIZO NINI? BEI YA MKAA", "WATUACHE TULALE"!

MANENO na misemo mingi inayoingia na kukaa kwenye vichwa vya watu na hasa watoto na vijana ambao ndiyo wengi, hutokana na nyimbo za wanamuziki, waigizaji kupitia kazi zao, matangazo maarufu ya biashara na maneno au kauli za watu wengine maarufu (Quotations) ikiwa ni pamoja na viongozi.

Kila wiki siku ya Jumamosi, Semadat blog itakuwa ikikuletea kilichozungumzwa mtaani na mtu yeyote kwa kuweka msisitizo au akizungumza katika hali ya utani kwa kutumia maneno au misemo hiyo.

Kwa kuanza, leo amekutwa kijana mmoja maeneo ya kona ya barabara ya kwenda Chuo kikuu cha Dar es Salaam jirani na Mlimani City jijini Dar es Salaam, ambaye ameonekana akiwa na mawazo mengi. Alipoulizwa "TATIZO NINI?", jamaa mmoja pembeni akajibu kwa utani "BEI YA MKAA". Baada ya dakika kadhaa akashuka dada mmoja kutoka kwenye  Bajaji akiongea kwa njia ya simu kwa sauti ya juu, maongezi ambayo ni kama alikuwa anapinga jambo flani. Ghafla akamalizia kwa kusema "WATUACHE TULALE", akaweka simu yake mfukoni na kuondoka.


"Week End" njema na endelea kutembelea SEMADAT (Hamasa ya Ubunifu).

Nick wa pili  " Bei ya mkaa"
Joe Makini
Diamond "Watuache tulale"

Friday, September 20, 2013

MWANZO WA NGOLOLO USIWE MWISHO WA KIDUKU

Diamond Platnumz akicheza Ngololo

SIKU zote jambo zuri sana linatokana na mazuri mengi. Nchi nyingi za Afrika zenye wasanii wanaojulikana kimataifa mfano Nigeria, Afrika kusini na nyinginezo, tayari zilishakuwa na wanamuziki idadi ya kutosha nchini mwao, nchi zinazoonekana kuwa na staili ya muziki unaozitambulisha tayali zilishakuwa na aina nyingi sana za muziki nchini mwao.  Kinachotokea ni kwamba aina flani ya muziki hutokea kupendwa zaidi hasa nje ya mipaka wanapotokea baadhi ya wanamuziki kuvuma zaidi nje ya nchi hizo lakini aina zingine pia huendelea kufanyika na hufanya vizuri pia. Ndivyo ilivyo pia kwenye staili za kucheza muziki.

Nchi ya Nigeria inavuma kwa 'Niger style' iliyotambulishwa na 2Face Idibia na ambayo pia inafanywa na kina P-Square, J-Martin na wengine. Hata hivyo ndani ya nchi hiyo wapo wanamuziki wengi wanaoendelea kufanya staili zingine ikiwa ni pamoja na Afro beat, wakifuata nyayo za wanamuziki kama Nico Mbarga mzee wa 'Sweet mother', Afro pop na nyinginezo. Huo ni mfano wa muziki na wanamuziki. 

Katika staili za kucheza utaona mfano mzuri jinsi gani Afrika Kusini staili za kucheza kwaito zinaongezeka, ipo ya kuyumba na kugeuka, alafu hatua kadhaa kushoto na kulia, pia ipo ile ya kunyoosha mikono, kushika kichwa, mabega na kuruka mbele na nyuma kama watoto wanacheza ule mchezo wa kuruka mistari kwenye vyumba vilivyochorwa udongoni, wengine wanaiita 'Modern kwaito dance style'.Zipo nyingi na zote bado zinatumika mpaka sasa. 

Pongezi sana kwa wote waliobuni na wanaoendelea kubuni staili za kucheza muziki hapa Tanzania, ikiwemo ile ya KIDUKU na NGOLOLO. Na kila kinachobuniwa kiendelee na kuenziwa ili katika mengi mazuri litokee la kukubalika zaidi mpaka kufahamika Ulimwengu mzima.
 Mwanamuziki wa Uingereza mwenye asili ya Ghana,Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki wa Tanzania

Thursday, September 19, 2013

DIAMOND NDANI YA MALAYSIA, OMMY DIMPOZI MAREKANI

 Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz

IMEKUWA ni jambo la kawaida sana kusikia wapenzi au mashabiki wa muziki na kazi zingine za sanaa wakilinganisha kazi zilizotoka au zinazovuma kwa kipindi au msimu mmoja, mara nyingi inatokea kwa kazi mbili au wasanii wawili. Ukiwa mtaani utasikia maneno kama "Huu wimbo wa msanii flani ni noma", mtu akimaanisha  wimbo flani ni mzuri sana, mwingine utasikia akisema "Ni noma lakini haushindi wa flani". Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa kazi za sanaa, nisikurudishe nyuma sana lakini kama utakumbuka kipindi cha ujio wa Marlaw na Ali Kiba kupitia nyimbo zao za 'Bembeleza' na 'Kigoma' utaelewa ninachosema na huo ni mfano tu. 

Hiyo hutokea sio tu kwa kazi za sanaa bali pia wasanii wenyewe. Ni jambo ambalo hutokea pasipo kupanga, kwamba wasanii  wawili wanaoendana kwa namna yoyote ile, mfano staili zao, maudhui au 'personality' zao wanapotoa kazi nzuri kwa msimu mmoja kazi hizo hugawana mashabiki(Fan base) na kuzua mijadara ya mashabiki.Hiyo pia ni ishara ya kukubalika.Ndicho kilichopo mitaani kwa sasa juu ya wimbo wa Diamond Platnumz 'Number one' na wimbo wa Ommy Dimpoz 'Bado Tupogo'. 

Diamond  anatarajia kuanza 'tour,yake ya kimuziki nchini Malaysia muda mfupi kuanzia sasa, pia Ommy tayari yuko nchini Marekani kwa ajiri hiyo.