UA-45153891-1

Tuesday, September 24, 2013

TAMASHA LA KWANZA LA FILAMU NCHINI TANZANIA KUANZA LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Vincent Kigos-RAY 


MTAYARISHAJI na muongozaji Bora wa filamu Swahilihood Vincent Kigosi ‘ Ray the Greatest’ ndiye“Nimefurahia sana kuchaguliwa kuwa ni 'Official Producer' na 'Director' wa tamasha kubwa la filamu linalojulikana kwa jina la Dar Filamu Festival (DFF 2013) lililoanza leo  tarehe 24 na ambalo litamalizika 26 September 2013,katika viwanja vya CoICT- UDSM- Posta Kijitonyama, katika kuhamasisha wapenzi wa filamu kutazama filamu za nyumbani.
   
Tamasha hilo limeandaliwa na kampuni ya Haak Neel Production kwa kushirikiana na mtandao wa habari za filamu wa Filamucentral, ambalo lina lengo la kutoa hamasa kwa jamii kuangalia filamu za Kiswahili.Mratibu wa tamasha hilo, Staford Kihore, alisema kuwa, kwa kuzingatia maendeleo ya filamu siku tatu za tamasha hilo, kila moja imepewa jina, ambako Septemba 24 ni siku ya Bongo Movie Classics, Septemba 25 ni‘Quality Nights’ na siku ya mwisho itakuwa ni ‘Stars Nights’.Alisema, tamasha hilo litapambwa na wasanii mbalimbali wakiongozwa na Vicent Kigosi ‘Ray’ na Elizabeth Michael ‘Lulu’.Aliongeza kuwa, tamasha hilo litahusisha filamu za Tanzania pekee na miaka ijayo watashirikisha kutoka sehemu mbalimbali zinazotumia lugha ya Kiswahili.

Naye Mkurugenzi wa Haak Neel Production, Geofrey Mahendeka alisema, Septemba 26 ni siku muhimu, kwani taasisi kama Mamlaka ya Mapato (TRA), Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza Tanzania, Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), na nyinginezo za usambazaji wa filamu zitakuwepo.

Kwa upande wake, Balozi wa Tamasha hilo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, amewaomba watanzania kuliunga mkono tamasha hilo na kuhakikisha linakuwa chachu ya maendeleo ya tasnia ya filamu nchini.Aliongeza kuwa, tamasha hilo litawakutanisha wasanii wote wa filamu na ni jukwaa litakalojenga, kutangaza na kuboresha tasnia ya filamu inayokua kila siku.Tamasha hilo litaambatana na utoaji wa semina kwa wadau wa filamu, ambako masomo ya uandishi wa muswada, uigizaji na uongozaji wa filamu yatafundishwa.

No comments:

Post a Comment