Mzee Gurumo na Diamond siku ya tukio hilo
Kwanza pongezi nyingi zimuendee
msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz kwa kitendo alichofanya siku
chache zilizopita wakati akizindua video mpya ya wimbo wake wa “Number one”.Pia
shukurani zenye ujazo wa kipekee zimuendee Mzee Gulumo kwa kuweka wazi, kwani
hakakulenga kumkatisha mtu tamaa aliposema anastaafu bila hata baiskeli, bali
kutoa changamoto kwa wanamuziki na sekta nzima inayohusu Sanaa. Hakika
wanamuziki hawa ni hamasa ya ubunifu.
Baada ya kutafakali kitendo
hicho, kwa mtazamo wangu, zawadi aliyotoa Diamond inazungumza mambo mengi kwa
watu tofauti.
Wadau wa sanaa na wafanyabiashara
Kutowasahau
wasanii wazee, wao pia wana umaarufu mkubwa na wakipewa nafasi kushiriki
kampeini mbalimbali na matangazo wanaweza kufanya vizuri katika nafasi
zao (Celebrity endorsement)
Wasanii wakongwe
Wasanii
wakongwe na hasa wa kizazi kipya wajenge tabia ya kuwaheshimu na kuwapa moyo
wasanii wanaochipukia hii inafanya wao pia waheshimike mara kumi zaidi ya kawaida.
Nakumbuka usiku flani msanii Chris Brown alikuwa akifanya onyesho kwenye tuzo
flani za muziki nchini Marekani. Justine Timberlake alipopata nafasi ya kuuzungumzia
usiku huo alisema yafuatayo ukumbini “When I see Chris Brown on stage, it
reminds me on how much I getting old”.Kwamba amuonapo Chris akifanya vitu vyake
jukwaani inamkumbusha jinsi gani yeye anaanza kuzeeka. Ni mara chache sana kwa hapa
Bongo kusikia maneno kama haya.
Wasanii wanaochipukia
Kujiandaa
kustaafu. Wafanyakazi walioajiriwa kwenye sekta rasmi huanza kujiandaa kustaafu baada tu ya mwezi wa
kwanza tangu wanapoanza kazi kupitia mifuko mbalimbali inayohifadhi kiasi flani
cha mshaara. Mbinu tofauti inaweza kutumika kwa kila msanii ikiwa ni pamoja na
kuwekeza. Kutobweteka na kuvimba vichwa mambo yanapowanyookea. Wakumbuke pia
kwamba siku za nyuma sanaa ilikuwa haijaanza kulipa kama sasa kutokana
kutokuwapo kwa utayarishaji bora wa kazi, uchache wa vyombo vya habari, uchache
wa matumizi ya sanaa na wasanii kwenye matangazo ya biashara, udhamini na
mengine mengi.
Mashabiki
No comments:
Post a Comment