UA-45153891-1

Sunday, September 8, 2013

STAILI YA AZONTO KAMA MADINI NCHINI GHANA

Fuse ODG


WAKATI mwanamuziki mkali wa staili ya Azonto kutoka Uingereza Fuse ODG akifanya vitu vyake hapa Bongo, bila shaka ungependa pia kufahamu asili na chanzo cha uchezaji huyo pamoja na heshima ambayo staili hiyo inapewa na nchi ya Ghana.

Staili ya Azonto ilianzia nchini Ghana. Ilitokana na uchezaji wa kiasili unaoitwa  Kpanlogo wa sehemu za pwani ya bahari nchini humo maeneo ya Teshia, Nugua , Tema na mengineyo, yote yakiwa ni sehemu ya Accra. Uchezaji wa Azonto unatokana na ishara za shughuri za kila siku za mikono kama vile kufua, kupiga pasi nguo, kujiweka sawa, mfano kuchana  nywele, kuvaa nguo, kusali,  kuendesha na shughuri mbalimbali za kimichezo kama Masumbwi, kuogelea na mingineyo.

Neno Azonto asili yake ni neno Azontoa ambalo maana yake ni msichana wa mtaani ambaye maisha yake si mazuri. Ilianza kutumika mwaka 1990 kwa ajiri ya kukosoa watu ambao walikuwa hawapendi ziongezwe shule za kike, au wasichana waende shule na hivyo kupata umaarufu nchini humo ilipokuwa ikitumika kwenye kampeini hizo. Kwa mara ya kwanza staili ya Azonto ilianza kupata umaarufu nje ya mipaka ya Ghana kupitia mtandao wa kijamii ya Youtube baada ya video ya watu waliokuwa wakicheza nyumbani kwao kuchukuliwa kikawaida na kuwekwa kwenye mtandao huo pasipokuwa na sababu za kibiashara.

Mpaka sasa kuna taarifa kwamba baada ya staili hiyo kukubalika na kuanza kutumika kwenye shughuri mbalimbali za burudani karibu Ulimwengu mzima, kimeundwa chombo maalum nchini Ghana kinachoitwa “Azonto Ghana Commission” ambacho kazi yake ni kuwaunganisha na kuwatambua wasanii maarufu wanaotumia staili hiyo. Pia kinatumika kama Idara ya kuinua vikundi vya asili na mtu yeyote mwenye uwezo wa kucheza miondoko hiyo. Ndicho chombo  kilichopewa pia jukumu la  kusimamia mkakati mzima wa kuitumia staili ya Azonto kuitangaza nchi ya Ghana, amani na mshikamano wa chi hiyo.

Fuse ODG mwenye asili ya Ghana ambaye anatamba kwa nyimbo za Azonto na Antenna ni miongoni pia mwa waliochangia kulitangaza jina la staili hiyo ya kucheza muziki.

Watoto na vijana wa nchini Ghana wakicheza Azonto
Wachezaji wa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya Ghana wakishangilia goli kwa kucheza  Azonto
                                                             
Vanessa Boateng wa Uingereza akimfundisha Prince Williams kucheza Azonto

No comments:

Post a Comment