UA-45153891-1

Monday, September 30, 2013

VANESSA MDEE- MWANASHERIA ANAYETUMIA VIPAJI VYAKE IPASAVYO




Vanessa  Mdee  alizaliwa Tanzania mwaka 1988 na kukulia New York, Paris, Nairobi na Arusha.

Japo alisoma sheria ‘Catholic  University of Eastern Africa’ ,ubunifu kupitia sanaa ndicho kitu ambacho kilikuwa tayari kiko kwenye damu yake. Tangu aliposhinda kwenye VJ search hapa nchini Tanzania mwaka 2007, vipaji vyake vingi vilizidi kuibuka na kumfanya asonge mbele zaidi.  Akiwa na umri wa miaka 19 tu Vanessa aliondoka nchini akiwa mtanzania wa kwanza kufanya kazi MTV akiungana na waendeshaji (VJs) wengine kwenye kipindi cha Coca Cola Chart.

Mwaka mmoja baada ya hapo Vanessa alifahamika sana kwenye sekta ya burudani Tanzania na bara zima la Afrika kwa kushiriki maonyesho mbalimbali nchini Nigeria, Afrika kusini, Kenya, Msumbiji, Angola, Uganda, Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo, Tanzania, Marekani na  Brazil.


Mwaka 2008 Vanessa alifanya kazi na “MTV Staying Alive Foundation” akishughurika na mambo mbalimbali za kijamii hasa yanayohusu vijana ambao wanataka kubadilika na kuleta mabadiliko kwenye jamii zao kupitia kazi za ubunifu ikiwa pamoja na muziki. Mwanzoni mwa mwaka 2009 alitangaza kwenye onyesho la “Senses, Sounds and Wisdom” katika tamasha la kimataifa la muziki  la Sauti Za Busara ambapo pia aliweza kujitambulisha kiutamaduni na mambo ya mitindo kupitia ‘Swahili Culture’ na ‘Vee-style’

Shughuri za mitindo zikamfanya awe mtangazaji kwenye matukio ya MAMA (MTV AFRICA MUSIC AWARD) kwa miaka 3 mfululizo, kabla hajawa mtangazaji wa redio Choice FM ya hapa nchini Tanzania. Ni mwanaharakati wa mapambano dhidi ya Ukimwi na mwakilishi wa UNAIDS, akihusika na habari juu ya janga hilo kupitia MTV na tovuti (website) yake.

Pia ni mwanamuziki ambaye anafanya vizuri kupitia nyimbo zake na zile alizoshirikishwa na wanamuziki wengine wa hapa nchini Tanzania.

 
Vanessa Hau Mdee, a.k.a. Vee akiwa studio na Ludacris

No comments:

Post a Comment