UA-45153891-1

Wednesday, September 18, 2013

MILLARD AYO- KUTOKA UFUNDI WA SATELLITE DISH, TV NA REDIO MPAKA UANDISHI WA HABARI NA UTANGAZAJI

UFUNDI wa Electronic ni kazi yake ya pili aliyoipenda lakini alivutiwa zaidi na shughuri za habari. Baada ya kumaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya sekondari Mbezi Beach, Millard alijiunga na Arusha College of Electronics na kusomea ufundi wa kutengeneza satellite dish, tv deck na radio wakati akisubiri matokeo. Kisha akapata nafasi ya kwenda kujiunga na East Africa Training Institute kusomea utangazaji na uandishi wa habari mwaka 2004.

Amefanya kazi za uandishi na utangazaji TVZ Zanzibar, Wapo Radio, ITV/Radio na sasa CLOUDS FM. Aliaza kazi pasipo kulipwa chochote mpaka baadae alipoaza kupokea  shilingi elfu 5 kwa wiki akiwa Wapo Radio.Anasema hii pia ilitokana na jinsi alivyoweza kujituma maana aliambiwa hatolipwa kwa sababu kanisa lililokua linamiliki Radio hiyo halikuwa na pesa kwa ajiri hiyo.

Ubunifu wake kupitia kipindi cha AMPLIFAYA pamoja na website yake ya millardayo.com ndivyo vilivyofanya ukubwa wa jina lake uongezeke.Mpaka sasa Millard Ayo anamiliki tuzo nyingi ikiwemo ya Mtangazaji bora 2006 kutoka Tanzania Radio Awards, Website bora 2012 kutoka Vodacom Tanzania na African Stars, na mwandishi pekee kutunukiwa  heshima kutoka kwenye familia ya Marehemu mwigizaji Steven Kanumba.

Anawashukuru watu wengi waliomfikisha hapo ikiwa ni pamoja na mama yake, Uncle wake Gabriel alieyemshawishi mama yake amruhusu Millard kufanya anachokipenda zaidi,Joseph Msami aligundua kipaji chake. Reginald Mengi, Joyce Muhavile, Godwin Gondwe,Julius Nyaisanga, Deogratius Rweyunga, Abdallah Mwaipaya na Isack Gamba ambao walikua kama wazazi/marafiki.Pia anatoa shukurani za dhati kwa Gardner G Habash, Reuben Ndege,Sebastian Maganga,Bosi wake Ruge Mutahaba na Mkurugenzi mkuu wa Clouds FM ambaye yeye anamuita Big Boss Joseph Kusaga.

Millard Ayo akiwa kwenye interview na mmoja kati ya wazee wa longtime Mbeya

No comments:

Post a Comment