UA-45153891-1

Monday, September 9, 2013

WEMA SEPETU, JOKATE MWEGELO NA LISA JENSENI WAENDELEA KUSHINDANISHWA

 Wema Sepetu

Mshindi wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, mshindi wa pili Jokate Mwegelo  pamoja na mshindi wa tatu Lisa Jensen wamejikuta wakipendekezwa kwenye mashindano ya kumtafuta staa wa kike Bongo mwenye mvuto ambaye hajaolewa. Warembo hawa ambao ni wabunifu na wanafanya vizuri kwenye  sekta ya burudani na mitindo, wamekuwa na historia ya kuhusishwa na matukio yanayowagusa wote kwa pamoja, ikiwa ni pamoja na  tetesi za kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanamuziki Diamond Platnumz.

Mashindano ya kumtafuta  staa huyo yanaendeshwa  na Global Publishers kupitia mpango wa  ‘Ijumaa Sexiest’ ambapo washiriki wengi wametajwa akiwemo Jackline Wolper, Genevieve Mpangala, loveness Malinzi Diva,  Zamaradi Mketema, Elizabeth Michael “Lulu”, Agnes Masogange na wengine wengi.
    Jokate Mwegelo
 
Lisa Jensen

No comments:

Post a Comment