UA-45153891-1

Friday, September 20, 2013

MWANZO WA NGOLOLO USIWE MWISHO WA KIDUKU

Diamond Platnumz akicheza Ngololo

SIKU zote jambo zuri sana linatokana na mazuri mengi. Nchi nyingi za Afrika zenye wasanii wanaojulikana kimataifa mfano Nigeria, Afrika kusini na nyinginezo, tayari zilishakuwa na wanamuziki idadi ya kutosha nchini mwao, nchi zinazoonekana kuwa na staili ya muziki unaozitambulisha tayali zilishakuwa na aina nyingi sana za muziki nchini mwao.  Kinachotokea ni kwamba aina flani ya muziki hutokea kupendwa zaidi hasa nje ya mipaka wanapotokea baadhi ya wanamuziki kuvuma zaidi nje ya nchi hizo lakini aina zingine pia huendelea kufanyika na hufanya vizuri pia. Ndivyo ilivyo pia kwenye staili za kucheza muziki.

Nchi ya Nigeria inavuma kwa 'Niger style' iliyotambulishwa na 2Face Idibia na ambayo pia inafanywa na kina P-Square, J-Martin na wengine. Hata hivyo ndani ya nchi hiyo wapo wanamuziki wengi wanaoendelea kufanya staili zingine ikiwa ni pamoja na Afro beat, wakifuata nyayo za wanamuziki kama Nico Mbarga mzee wa 'Sweet mother', Afro pop na nyinginezo. Huo ni mfano wa muziki na wanamuziki. 

Katika staili za kucheza utaona mfano mzuri jinsi gani Afrika Kusini staili za kucheza kwaito zinaongezeka, ipo ya kuyumba na kugeuka, alafu hatua kadhaa kushoto na kulia, pia ipo ile ya kunyoosha mikono, kushika kichwa, mabega na kuruka mbele na nyuma kama watoto wanacheza ule mchezo wa kuruka mistari kwenye vyumba vilivyochorwa udongoni, wengine wanaiita 'Modern kwaito dance style'.Zipo nyingi na zote bado zinatumika mpaka sasa. 

Pongezi sana kwa wote waliobuni na wanaoendelea kubuni staili za kucheza muziki hapa Tanzania, ikiwemo ile ya KIDUKU na NGOLOLO. Na kila kinachobuniwa kiendelee na kuenziwa ili katika mengi mazuri litokee la kukubalika zaidi mpaka kufahamika Ulimwengu mzima.
 Mwanamuziki wa Uingereza mwenye asili ya Ghana,Fuse ODG akifundishwa kucheza kiduku na shabiki wa Tanzania

No comments:

Post a Comment