Muhidin Issa Michuzi akizungumza jambo kwenye moja ya makongamano
UKITEMBELEA mtandaoni utakutana
na neno
'Michuzi' kwa majina mengine tofauti na Issa Michuzi mmiliki wa Michuzi
Blog. Ni Blogs au maarufu kama Blogu zinazomilikiwa na watanzania wengine
wanaotokea katika familia moja na Blogger huyo mkongwe Muhidin
Issa Michuzi.
Safari yake ilianza kwa kupenda kazi ya kupiga picha na kusomea fani hiyo
miaka ya 80. Akiwa anaendelea na shuguri zake, siku flani moja ya picha zake ikachaguliwa kuingia
kwenye ukurasa wa mbele wa gazeti la serikali
la Daily News , akaendelea kufanya kazi
na gazeti hilo na kisha kuajiriwa kabisa na chombo hicho cha habari mwanzoni
mwa mwaka 1990. Baadae aliongeza taaluma ya ‘Photojournalism’ mjini Berlin
na uandishi wa habari Chuo kikuu cha Dar es Salaam na kumaliza
mwaka 1996.
Alianza kazi
ya Blogu mwaka 2005 ambapo kwa mara ya
kwanza Blogu yake iliingia mtandaoni Septemba 8, 2005. Lengo lake kuu ikiwa ni
kuwapa watu habari zinazohusu nchi ya Tanzania kupitia Blogu ya picha “photoblog”.
Mpaka sasa anamiliki tuzo nyingi ikiwa
ni pamoja na Blogu inayoongoza Tanzania kutoka ‘1st Annual Tanzanian Blog
Awards’, Blogu bora ya habari za siasa
mwaka 2011 kutoka ‘VADE Local Digital Media’ na ‘Vodacom
Awards for Digital Excellence’ mwaka 2012.
Ndugu zake ambao pia wanafahamika kama
Bloggers ni Ahmad and Othman na pamoja wameanzisha kampuni ya habari ambayo
inaitwa Michuzi Media Group (MMG).
.
No comments:
Post a Comment