UA-45153891-1

Friday, September 13, 2013

‘BADO TUPOGO’ (BADO TUPO NA TUNA-GO)-HAPPYBIRTHDAY OMMY DIMPOZ

Staa wa wimbo wa ‘Bado tupogo’ Faraji Nyembo ‘Ommy Dimpoz’, leo tarehe 13 Septemba 2013, anasherehekea siku yake ya kuzaliwa. Ommy ameuzungumzia pia wimbo wake huo mpya ambao alimshirikisha J-Martin kwamba Tupogo ni kifupi cha maneno Tupo na ‘Tuna-go’, tuna-go kwa maana ya tunaenda.

Akifunguka kupitia DoubleXL ya Clouds FM  leo hii, amesema wimbo huo unafanya vizuri sana ndani ya Tanzania, Africa Mashariki na ameambiwa na J-Martini kwamba umeanza pia kuwa mkubwa jijini Lagos nchini Nigeria. Amemshukuru AY kwa kumuunganisha na J-Martin kupitia Agency ya P-UNIT.

Ommy Dimpoz anatarajia kuendelea na ‘tour’ nchini Marekani, ambayo inadhaminiwa na Swahili Radio ya nchini humo pamoja na Voice of America (VOA).
Ommy Dimpoz akiwa na Ally Kiba wakati wa kupokea tuzo yake ya kwanza kupitia wimbo wa Nai nai mwaka 2012.

No comments:

Post a Comment