UA-45153891-1

Monday, September 16, 2013

LEO DUNIANI-SEPTEMBA 16-TAREHE YA KIHISTORIA KWA KAMPUNI YA APPLE, KUONDOKA NA KURUDI KWA STEVE JOB

Steve Job
SEPTEMBA 16 ambayo ni tarehe ya leo, ni ya kihistoria kwenye maisha ya  aliyekuwa Afisa Mtendaji mkuu (C.E.O) wa kampuni ya Apple Computers, Steve Job na kampuni yenyewe.

Tarehe kama hii mwaka 1985, ndiyo siku ambayo Steve Job aliacha kazi kwenye kampuni aliyoianzisha mwenyewe na kuwaachia wengine na kIsha kuirudia baada ya miaka 12 tarehe hiyo hiyo mwaka 1997.

Miaka michache baada ya kuanzisha kampuni ya Apple, Steve Job na rafiki yake Steve Wozniak walitafuta namna ya kuiendeleza kampuni kibiashara kwa kuajiri watu wenye ujuzi wa aina mbalimbali kwa ajiri ya usimamizi, akiwemo John Sculley mzoefu wa shughuri za masoko kutoka kampuni ya Pepsi Cola. Baadae bodi ya kampuni hiyo ilimpa mamraka makubwa John Sculley kama C.E.O kwa mtazamo kwamba Steve Job hatabiriki katika mambo ya uongozi. Steve Job alijiuzuru na kwenda kuanzisha kampuni yake nyingine ambayo aliipa jina la NeXT Inc. Kampuni hiyo ilianza kufanya mambo makubwa na ya kisasa wakati Apple ikianza kushuka. Ndipo Steve akaanza kutafutwa kwa hudi na uvumba ili awe  japo mshauri.

Mwaka 1996, kampuni ya Apple ikiwa chini ya C.E.O mpya Gil Amerio iliyanunua makampuni mawili ya Steve Job ambayo ni NeXT na NeXTSTEP wakati huo Steve akimiriki makampuni zaidi ya matatu ikiwa ni pamoja na Pixar iliyohusika zaidi na masuala ya Teknolojia za utayarishaji wa Filamu na Muziki ambayo ilikuwa tayari imetengeneza Filamu ya 'Toy Story' kupitia Studio yake ya Pixar Animation.

Hatimaye Septemba 16 1997 Steve Job alitangazwa kama C.E.O mpya wa Kampuni ya Apple ili akayafanye mambo yote ndani ya Kampuni hiyo. Ulimwengu ukaanza kuzungumza habari za iMac, iTunes, iPod, iPhone, iPad na mengine mengi.

Steve Job alizaliwa Februari 24 1955 na kufariki Dunia Octoba 5, 2011. Anakumbukwa kama Mjasiliamali aliyeleta mabadiliko makubwa kwenye Teknolojia na matumizi yake, yakiwemo ya sanaa kama utayarishaji wa Muziki, Filamu, usanifu wa kurasa za tovuti na ubunifu wa hapa na pale. Alipewa majina mengi kama "Design perfectionist", Creative thinker, "visionary", "Father of the Digital Revolution" na mengine mengi.

Picha za Steve Job akiwa na mzoefu wake wa masoko wa mwanzo John Sculley 

Ni 'LEO DUNIANI' ya Semadat.

No comments:

Post a Comment