UA-45153891-1

Thursday, September 19, 2013

DIAMOND NDANI YA MALAYSIA, OMMY DIMPOZI MAREKANI

 Diamond Platnumz na Ommy Dimpoz

IMEKUWA ni jambo la kawaida sana kusikia wapenzi au mashabiki wa muziki na kazi zingine za sanaa wakilinganisha kazi zilizotoka au zinazovuma kwa kipindi au msimu mmoja, mara nyingi inatokea kwa kazi mbili au wasanii wawili. Ukiwa mtaani utasikia maneno kama "Huu wimbo wa msanii flani ni noma", mtu akimaanisha  wimbo flani ni mzuri sana, mwingine utasikia akisema "Ni noma lakini haushindi wa flani". Ndugu msomaji na mfuatiliaji wa kazi za sanaa, nisikurudishe nyuma sana lakini kama utakumbuka kipindi cha ujio wa Marlaw na Ali Kiba kupitia nyimbo zao za 'Bembeleza' na 'Kigoma' utaelewa ninachosema na huo ni mfano tu. 

Hiyo hutokea sio tu kwa kazi za sanaa bali pia wasanii wenyewe. Ni jambo ambalo hutokea pasipo kupanga, kwamba wasanii  wawili wanaoendana kwa namna yoyote ile, mfano staili zao, maudhui au 'personality' zao wanapotoa kazi nzuri kwa msimu mmoja kazi hizo hugawana mashabiki(Fan base) na kuzua mijadara ya mashabiki.Hiyo pia ni ishara ya kukubalika.Ndicho kilichopo mitaani kwa sasa juu ya wimbo wa Diamond Platnumz 'Number one' na wimbo wa Ommy Dimpoz 'Bado Tupogo'. 

Diamond  anatarajia kuanza 'tour,yake ya kimuziki nchini Malaysia muda mfupi kuanzia sasa, pia Ommy tayari yuko nchini Marekani kwa ajiri hiyo.

No comments:

Post a Comment