MWANAMITINDO wa Tanzania anayefanya vizuri kwenye kimataifa Flaviana Matata, ameendelea kutamba katika fani hiyo baada ya kuonekana kwenye bango la mitindo la mbunifu Kenneth Cole nchini Marekani.
Flaviana Matata ambaye alizaliwa mwaka 1988 mkoani Shinyanga, ni mshiriki wa kwanza kutoka Tanzania kushindana katika Miss Universe 2007 na kuwa mshindi wa 6 kati ya washiriki 15. Ameshatokea kwenye machapisho mengi ya matangazo ya Sherri Hill, mwanamitindo maarufu wa kimarekani na mfanyabiashara mkubwa ambaye anatengeneza na kuuza magauni ya washiriki wa mashindano ya urembo na mavazi ya usiku.
Machi 2011 alishinda tuzo ya Arise Magazine kama mwanamitindo wa mwaka kwenye wiki ya mitindo ya Lagos nchini Nigeria. Pia ameuza sura katika majarida ya Dazed & Confused na i-D ya nchini Uingereza, Glass la Marekani na L'Officiel la Ufaransa. Matata pia alishafanya baadhi ya “modeling runway” kwa bidhaa kama za Mustafa Hassanali, Vivienne Westwood, Tory Burch, Suno, na Louise Gray na pia amehusika katika filamu ya Alexander McQueen ya aliyekuwa mwanamitindo wa Uingereza na kwenye tangazo la kampeni ya Spring Topshop mwaka 2011, bila kusahau shughuri zake nyingi anazofanya kupitia Flaviana Matata Foundation.
No comments:
Post a Comment