UA-45153891-1

Saturday, September 14, 2013

'FURSA' NA 'TWENDE ZETU'- DODOMA IDODOMYA

Maneno yanayotamba kwenye msimu wa Fiesta mwaka huu yaani 'Fursa' na 'Twende zetu' yaliendelea kusikika jana kwenye semina mkoani Dodoma na kusikilizwa na wananchi wengi wa mkoani humo. Maneno hayo ambayo yanahamasisha watanzania kutumia rasilimali walizonazo kujikwamua kutoka katika umasikini au kwa lugha ya sasa ya vijana 'KUTOKA', yaliambatana na tamasha kali la muziki kama ilivyofanyika katika mikoa mingine hapa nchini.
 Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba,akiongea jambo mbele ya wakazi wa Dodoma waliojitokeza kwenye Semina.
Mtangazaji wa Clouds FM, Millard Ayo akihamasisha wakazi wa Dodoma kutokata tamaa huku akitoa mifano juu ya yeye alikotoka na alipo sasa.
Burudani kutoka kwa Recho
  Mambo ndivyo yalivyokuwa

No comments:

Post a Comment