1. MISS WORLD
Hili ndilo
shindano kubwa kuliko yote ulimwenguni lilianzishwa mwaka 1951 nchini Uingereza
na mjasiliamali Erick Morley akiwa na mke wake Julia Morley. Ndilo shindano
lenye umaarufu kushinda yote na linalotangazwa na vyombo ya habari vingi
ulimwenguni. Kwa mwaka huu litafanyika Septemba 28 jijni Bali, nchini Indonesia. Nchi ya Tanzania inawakilishwa na Brigitte Alfred.
Miss Tanzanai 2012- Brigitte Alfred.
Hili ndilo shindano linalofuatia baada ya MissWord.
Lilianzishwa mwaka 1952 nchini Marekani na kampuni ya mavazi ya Pacific Mills
jimboni Calfornia kabla ya kumilikiwa na Donard Trump. Lilibadilishwa jina
kutoka Miss Universe Inc na kuitwa Miss Universe Organization mwaka 1998 na
makao yake makuu yakaamishwa kutoka Los Angeles,
California, kwenda New York . Kwa hapa Tanzania, aliyeshinda mwaka jana (2012)
kushiriki mashindano hayo ni Winfrida Dominic.
Miss Universe Tanzania 2012-Winfrida Dominic.
3. MISS INTERNATIONAL
Ni shindano la urembo lililoanzishwa nchini Marekani
mwaka 1960 jimboni California na kuhamishiwa jijini Tokyo nchini Marekani
ambako ndiyo makao makuu yake.Mwaka 2011, Tanzania iliwakilishwa na mrembo
Nelly Kamwelu ambaye pia kwa mwaka huo huo alishiriki mashindano matatu kuiwakilisha
Tanzania, ambayo ni Miss
Universe Tanzania ,Miss
Southern Africa International na Miss
International 2011.
Miss International Tanzania-Nelly Kamwelu
4. MISS EARTH
4. Ni
miongoni mwa mashindano makubwa manne ya urembo duniani. Lianzishwa mwaka 2001
na liko chini ya Miss
Earth Foundation. Lilianzishwa kwa ajiri ya kuhamasisha
utunzaji wa mazingira na mshindi wa shindano hilo ndiye msemaji wa Miss
Earth Foundation na
shirika la uratibu wa shughuri za mazingira la umoja wa mataifa(UNEP)
na mashirika mengine ya mazingira. Aliyeshinda mwaka 2012 kuiwakilisha Tanzania
kwenye shindano hilo ni Bahati Chando.
Miss Earth Tanzania 2012- Bahati Chando.
5. MISS
TOURISM (MISS UTALII)
Ni
miongoni mwa mashindano maarufu ya urembo ulimwenguni, Kwa mara ya kwanza
Tanzania ilifanya vizuri katika shindano hilo ambapo mshiriki Nelly Kamwelu ambaye alikuwa mshindi wa 5. Aliyeshinda
mwaka 2012 kuiwakilisha Tanzania kwenye shindano hilo ni Hadija Saidi
Mswaga.
Miss Tourism Tanzania 2012/2013-Hadija Saidi
Mswaga.
No comments:
Post a Comment