Jengo la World Trade Center likiungua moto
Jumatano ya 11/09/2013 ni siku ya kumbukumbu ya tukio la shambulizi la jengo
kubwa la kibiashara la nchini Marekani la World Trade Center (WTC) pamoja na
maeneo mengine muhimu ya nchi hiyo.
Semadat inakuletea
baadhi ya athali zilizotokea kwenye sekta ya habari na burudani nchini humo
kipindi hicho cha kuelekea mwishoni mwa mwaka 2001.
Televisheni
Kwa mara ya kwanza tangu kifo cha Raisi Kennedy, Televisheni
zote nchini Marekani zilitangaza kwamba hakutakuwa na matangazo ya biashara
wala vipindi vya burudani.
Kutokana na uzito wa tukio, waandishi wa habari walikuwa
wengi wakigombania taarifa mpaka vyombo vingi na hata vyenye majina makubwa
kutoa taarifa zisizo sahii wakati mwingine.
Mke wa Raisi Bush aliwatangazia wazazi wasiruhusu watoto wao
wadogo kutizama TV, akitoa angalizo
Kutokana na sababu za kihistoria kwamba kuna tukio lililowai
kutokea siku za nyuma ambalo picha zake ziliwaadhili
watoto waliotizama na kuwajengea hasira na chuki.
Redio
Uzinduzi wa Redio ya XM uliokuwa ufanyike tarehe 12 Septemba
2001 ulisogezwa mbele mpaka tarehe 25
Septemba 2001.
Waongozaji wa vipindi vya Redio walibadilisha mpangilio wa
vipindi vya muziki (Playlist) na program zingine.
Filamu
Filamu zisizopungua 45 zilizokaribia kutoka zilirudiwa
kufanyiwa uhariri (Editing) hasa zile ambazo picha za jengo hilo kabla
halijaharibiwa zilikuwa sehemu ya filamu hizo.Mfano ile ya Spider Man.
Baadhi ya filamu ilibidi zibadilishwe kuwa ‘series’ ili
kuleta hali ya uhalisia wa matukio, kabla jengo halijaharibika, wakati
limeharibika na wakati limetengamaa.
Muziki
Muda wa kutoa tuzo mbalimbali za muziki ulisogezwa mbele,
mfano tuzo za Grammy za 44.
Video mbalimbali za muziki zilizokuwa katika utayarishaji
zilirudiwa kwa kuchukua picha zingine au kuondoa baadhi ya picha. Mfano, bendi
ya Blink 182 ilirudia kuchukua picha za video za wimbo wa ‘Stay together for
kids’ baada ya kugundua kwamba kuna tukio kwenye picha za video hiyo ambalo limeendana na tukio halisi
la World Trade Center.
Studio ya Radio ya XM ya nchini Marekani ambayo uzinduzi wake ulisogezwa mbele kufuatia tukio hilo
Picha ya sehemu ya juu ya kasha la DVD ya Filamu ya Spider-man ambayo ni miongoni mwa zile zilizorudiwa kufanyiwa 'editing' baada ya shambulizi hilo,
Picha ya sehemu ya juu ya kasha la CD ya bendi ya muziki ya Blink-182 ambayo video ya wimbo wake wa 'Stay together for kids’ ilirudiwa kuchukuliwa baadhi ya picha.
No comments:
Post a Comment