UA-45153891-1

Wednesday, April 2, 2014

DIAMOND PLATNUMZ AZUNGUMZIA KAMPENI YA KILIMO YA ONE.ORG INAYOITWA'Do Agric'


Msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz ambaye ni miongoni mwa wanamuziki 19 wa Afrika waliochaguliwa kukutana  nchini Nigeria ili kushiriki katika wimbo wa pamoja wa kuhamasisha vijana kujiunga na kilimo, amesikika akizungumzia kampeni hiyo leo kupitia Clouds FM. 

"Kilimo si ushamba, tajiri wa kwanza Afrika Aliko Dangote ni mkulima pia. Unaweza kuwa na shughuri zako mjini lakini ukawa mkulima pia kupitia watu uliowaajiri ambao wanafanya kazi moja kwa moja shambani, inawezekana pia kwa watu kama sisi ambao wengine wanatuita wauza sura", alisema Diamond ambaye pia akiwa jijini Lagos, amefanikiwa kumalizia wimbo wake anaofanya na staa wa nchini humo 'Iyanya' ambaye alikuwa hapa nchini Tanzania mwaka jana katika msimu wa Fiesta.

MR NICE BADILI MATUKIO HASI KUWA CHANYA



Sina uhakika kama uko facebook, twitter, Insatagram au kwingine niweze hata kushauri chochote kupitia akaunti yako. Labda tu niseme kupitia semadat, sina shaka waweza pata ujumbe huu kupitia watu wengine ambao uko karibu nao na wako mtandaoni. Kaka  umaarufu wako ni mkubwa sana. Mpaka mwanzoni mwa mwaka jana, wewe na  Saida Kalori ndiyo wasanii pekee wa muziki wa Tanzania mliokuwa mkitolewa mifano mpaka na viongozi wataalam wa masoko katika mada mbalimbali za nembo au alama  mashuhuri za watu kwa kuzungumzia mtu mmoja mmoja au kwa lugha ya Kiingereza wanasema 'Personal Branding'.

TUNDAMANI ATAKIWA KUWA MZALENDO


Wakati vyombo kadhaa vya habari vikihubiri Uzalendo na Amani, msanii wa Bongo Flava ambaye kwa sasa anatamba na wimbo wa Msambinungwa, ameonekana kuwa tofauti baada ya mwanadada mmoja anayeitwa Esta kuweka wazi kwamba picha za video ya wimbo huo hazikuchukuliwa  jijini Nairobi kama mwanamuziki huyo alivyosema, bali shughuri hiyo ilifanyika hapa hapa nchini Tanzania kwenye studio inayoongozwa na mwanadada huyo mjasiliamali. 

Tuesday, April 1, 2014

RAMANI YA DUNIA KAMA ILIVYOKUTWA MTANDAONI


BONGO QUEEN LEO NDANI YA SEMADAT

Leo tuko na muimbaji katika muziki wa kizazi kipya yaani  Bongo Flava ambaye anaitwa Linah Sanga. Anatokea katika nyumba ya vipaji THT. Huwezi kuwataja waimbaji bora wa kike nchini Tanzania pasipo kumtaja. Yuko katika tuzo za KTML 2014 kipengele cha muimbaji bora wa kike.

SEMADAT NA WAWILI KWA PICHA- JACKLINE WOLPER NA JOKATE MWEGELO


AGNES GERALD 'MASOGANGE' KUSHIRIKI VIDEO MPYA YA 50 CENT NCHINI MAREKANI


Muigizaji maarufu wa video za muziki 'video vixen' wa hapa Tanzania, Agnes Gerald 'Masogange' ataondoka kwenda nchini Marekani kwa ajili ya kushiriki kwenye video mpya ya mwanamuziki mahiri wa Hip hop nchini Marekani '50 Cent'. Mwanadada huyo ambaye amefanya video za wanamuziki kadhaa wa hapa nchini ikiwa pamoja na za nyimbo kama 'Masogange' wa Belle 9 na 'Nangoja ageuke' wa Mwana FA, ameitwa nchini Marekani kwa ajili ya shughuri hiyo baada ya kuonekana kupitia mtandao wa kijamii wa Youtube kwenye moja ya video za muziki wa Bongo Flava.

Agnes Gerald katika picha zaidi:

Thursday, March 27, 2014

HAPPY BIRTHDAY MARIAH CAREY


Staa huyu wa "We Belong Together" ametimiza miaka 44 leo.

GARI ALILONUNUA MASANJA MKANDAMIZAJI


Mchekeshaji hodari hapa nchini Tanzania maarufu kama 'Masanja Mkandamizaji' ambaye ni miongoni mwa watanzania waliofanikiwa kupitia sanaa, amenunua gari hili, kama linavyoonekana kwenye picha hapa chini.

BONGO QUEEN LEO NDANI YA SEMADAT


Leo tuko na mwanamuziki machachari wa kike 'Snura Mushi' ambaye ana nyimbo zenye maudhui ya pekee. Ukisikiliza wimbo wake hata kama ni mpya utajua ni yeye kutokana na mpangilio wa mashairi yake. Ni mbunifu ambaye amejitengenezea alama ya pekee kimuziki. Alianza na "Majanga", ikafuata "Nimevurugwa" na sasa ni "Ushaharibu".

SEMADAT NA WAWILI KWA PICHA- RIHANNA NA OPRAH WINFREY


REDD'S MISS TANZANIA YAWAHASA MAWAKALA WAKE KUTOAHIDI ZAWADI BILA KUTOA

Mawakala wa Redd's Miss Tanzania wakiwa kwenye semina

Waandaaji na wadhamini wakuu wa shindano maarufu hapa nchini la Miss Tanzania, wamewahasa mawakala  wanaohusika na mashindano hayo ngazi za awali zikiwemo za vitongoji kutoahidi zawadi ambazo ni juu ya uwezo wao na hivyo kushindwa kutoa pindi washindi wanapopatikana.

Wednesday, March 26, 2014

MAONI YA MADEE NA SNURA BAADA YA NYIMBO ZAO KUTOINGIA KTMA KWA SABABU ZA KIMAADILI

Madee

Baada ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kutangaza majina ya wanamuziki na nyimbo zilizoingia kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro, ikiwa ni pamoja na kuwataja wasanii ambao nyimbo zao hazikupata nafasi hiyo kutokana na sababu za kimaadili, wasanii hao wamesikika kupitia vyombo  vya habari wakitoa maoni yao juu ya suala hilo.

BONGO QUEEN LEO KATIKA SEMADAT


Leo tuko na mwanadada Wastara Juma, ni muigizaji wa Bongo Movie anayeendelea kufanya vizuri katika tasnia hiyo pamoja na changamoto mbalimbali alizokutana nazo ikiwa ni pamoja na kuuguliwa na kuondokewa na mumewe marehemu Juma Kilowoko ‘Sajuki’ . Anajiamini na anaendelea kulisukuma gurudumu la sanaa vilivyo.

USHAURI WA MASOUD KIPANYA


Ameshauri hivi jana Machi 25, 2014 kupitia ukurasa wake wa Facebook:

SEMADAT NA WAWILI KWA PICHA-LEO NI NANCY SUMARI NA KHADIJA MWANAMBOKA


HII NI MIONGONI MWA KEKI ZA 'BIRTHDAY' ZILIZOLIWA MWEZI MACHI 2014


Ilikuwa siku ya kuzaliwa ya mwanamitindo flani hapa nchini Tanzania tarehe 20, Machi 2014. Tazama picha zinazofuata kujua ni nani.

Tuesday, March 25, 2014

MAJINA YA WALIOINGIA KTMA 'KILIMANJARO TANZANIA MUSIC AWARDS 2014' YATANGAZWA

LADY JAYDEE NA  DIAMOND PLATNUMZ WAONGOZA KWA KUTAJWA
Yafuatayo ni majina ya wasanii na nyimbo katika vipengele:

WIMBO BORA WA MWAKA
Number One – Diamond
Joto Hasira – Jaydee
I love u – Cassim
Yahaya – Lady Jaydee
Kidela – Abdul Kiba
Muziki Gani – Nay wa Mitego

Monday, March 24, 2014

HARUSI YA PAUL OKOYE WA P-SQUARE NA ANITA ISAMA ILIVYOKUWA HUKO NCHINI NIGERIA



Ilikuwa siku kubwa kwa Paul Okoye wa P-Squre na mpenzi wake wa muda mrefu Anita Isama katika Harusi ya kiutamaduni iliyofanyika wikend iliyopita, siku ya Jumamosi Machi 22, 2014. 

Upambaji wa ukumbi ulifanywa na wataalam wa fani hiyo nchini Nigeria wanaoitwa 'Wedding Guru' ambao pia ndiyo walihusika katika Harusi ya pacha wake Paul, yaani Peter, iliyofanyika mwishoni mwa mwaka 2013.  

Mastaa waliokuwepo katika Harusi hiyo ni pamoja muigizaji Omotola Jalade, wanamuziki Iyanya, Banky, Peter Okoye ambaye ni pacha wake Paul pamoja na kaka yao Jude Okoye. Tazama picha za kutosha hapa:

Friday, March 21, 2014

BONGO QUEEN LEO KATIKA SEMADAT


Leo tuko na mwanadada Hamisa  Hassan Mobeto ambaye anafanya jambo flani  kila mwaka juu ya fani yake ya mitindo tangu alipoanza mwaka 2010. Anatajwa na mtandao wa jarida la VIBE kama mtu wa kuangalia sana mwaka huu katika fani ya mitindo. Binti huyu mwenye umri wa miaka 21 ambaye  anatokea Mwanza , alianzia safari yake katika shindano ya XXL Back To School  ambapo aliibuka mshindi mwaka 2010. 

HUYU NDIYE MBWA ALIYENUNULIWA BEI YA JUU KULIKO WOTE DUNIANI - ZAIDI YA $1.9 MILIONI



Mbwa mwenye umri wa mwaka mmoja aina ya "Tibetan mastiff" aliyeuzwa nchini China kwa karibu dola za kimarekani milioni 2, inasemekana ndiye mbwa aliyeuzwa kwa bei kubwa kuliko wote ulimwenguni mpaka sasa kwa mujibu wa gazeti la New York Daily News. Mbwa huyo aliuzwa kwenye maonyesho ya kifahari huko Hangzhou mashariki mwa China.

SEMADAT - WAWILI KWA PICHA-ELIZABETH MICHAEL 'LULU' NA MAMA KANUMBA


llikuwa ni siku ya kuzaliwa mama Kanumba siku kadhaa zilizopita.

RONALDINHO ‘GAUCHO’ ATIMIZA MIAKA 34 (HAPPY BIRTHDAY GAUCHO)


Mwanasoka maarufu wa nchini Brazil ambaye mwanzoni mwa mwaka huu alisema atakapoachana na mchezo wa Soka ataingia kwenye sanaa ya muziki, Ronaldinho ‘Gaucho’ anasherehekea siku yake ya kuzaliwa leo Machi 21, 2014 ambapo anatimiza miaka 34.

SIKU YA USHAIRI ULIMWENGUNI ‘WORLD POETRY DAY’

Mrisho Mpoto: Mmoja wa watunzi maarufu wa mashairi  nchini Tanzania

Machi 21 ni siku ambayo ilitambuliwa rasmi na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni ‘UNESCO’ kuanzia mwaka 1999, kama siku ya Ushairi ulimwenguni. Umuhimu wa siku hii ni kuhamasisha usomaji, uandishi, uchapishaji na kufundisha  ushairi ulimwenguni. Semadat inakutakieni heri ya siku ya ushairi duniani.

D' BANJ AZINDUA BIDHAA YAKE INAYOITWA KOKO GARRI


Mwanamuziki wa nchini Nigeria, star wa wimbo wa Oliver twist, ambaye ni miongoni mwa wanamuziki 10 bora matajiri barani Afrika kutokana na muziki na biashara zingine, amezindua bidhaa yake mpya inayoitwa Koko Garri. Bidhaa hiyo inayotokana na mazao ya kilimo imezinduliwa na mwanamuziki huyo jana Machi 20, 2014 ndani ya jiji la Abuja. 

Thursday, March 20, 2014

SIKU YA FURAHA YA KIMATAIFA (INTERNATIONAL DAY OF HAPPINESS, 20 MARCH 2014)


"Furaha inaweza kuwa na maana tofauti kwa watu tofauti lakini wote tunaweza kukubaliana kwamba inamaanisha kufanya kila linalowezekana kumaliza migogoro, umasikini na hali zingine mbaya ambazo binadamu wenzetu wengi wanaishi nazo".  Ni ujumbe kutoka kwa Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa  Ban Ki-moon, katika siku hii ya furaha duniani Machi 20, 2014.

PICHA 20 ZA MANENO NA UJUMBE WA HAMASA KUTOKA 'ADDICTED TO SUCCESS.COM'


Kwa  wale mnaopenda kusoma ujumbe wa dizaini flani na pia kutupia Facebook na pande zingine za mitandao ya kijamii. Hapa ni mzigo wa picha 20 kwa hisani ya mtandao wa 'Addicted to success.com'.

HARUSI YA PAUL WA P-SQUARE NA ANITA BADO SIKU MBILI TU!

Harusi ya kiasili ya mwanamuziki pacha wa kundi la P-Square Paul Okoye na mchumba wake Anita Isama ambayo itafanyika mwezi huu pande za Port Harcourt nchini Nigeria, imebakiza siku mbili tu. Harusi hiyo itafanyika Jumamosi Machi 22, 2014. Wawili hao wamekuwa na maandalizi makubwa juu ya harusi hiyo na wanafamilia wao walishaanza muda mrefu kusambaza kadi za mialiko.

"Nimehamua, nimekwisha iandaa akili yangu, sasa unakaribia muda wa mtu kutulia", Ndivyo Paul alivyoandika kwenye akaunti yake ya mtandao wa Instagram. Hizi ni baadhi ya picha za wawili hao wakati wakisubiri kwa hamu harusi hiyo.

PICHA KUMI ZA JACK PATRICK CLIFF ZILIZOVUMA KUANZIA JANUARI 2014


Endelea....

MSHINDI WA BBA 2013 DILLISH MATHEW AONYESHA PETE YAKE YA UCHUMBA



Baada ya uhusiano aliokuwa nao na mpenzi wake Stephen anayeonekana nae kwenye picha kuvunjika siku ya Februari 14, 2014, sasa ameonyesha pete aliovishwa na mwingine. Ni kupitia mtandao wa Instagram ambapo pia alisema hivi:

BONGO QUEEN LEO KATIKA SEMADAT


Leo tuko na muigizaji wa kike wa muda mrefu ambaye watu wengi wanamfahamu kama zao la kundi la Kaole, si mwingine bali ni Brandina Chagula 'Johari'. Ni miongoni mwa wasanii wa kike wanaofanya kazi kwa bidii ambaye pia ana hisa kwenye kampuni ya RJ inayoshughurika na utayarishaji wa filamu za Bongo.

Tuesday, March 11, 2014

HUWEZI KUIPENDA AFRIKA KAMA HUJAIPENDA TANZANIA NA HUWEZI KUIPENDA TANZANIA KAMA HUJAPENDA CHIMBUKO LAKO NDANI YA TANZANIA

Semadat  inawapa tano wote wanaokumbuka walikotoka ikiwa pamoja na wale wasanii wa Bongo Flava na Hip hop wanaoipa mashavu mikoa yao. Kulia na Izzo Business kutoka Mbeya ambaye siku chache zilizopita aliachia wimbo unaoitwa "TUMMOGHELE". Wapo wengine ambao wanatangaza sana majina ya mikoa yao akiwemo, Fid Q, Afande Sele, Joh Makini na wengine. Sanaa inaambatana na uzalendo na uzalendo una asili yake.

CHRISTIANO RONALDO ATANGAZWA MWANASOKA TAJIRI KULIKO WOTE DUNIANI (€148M ), MESSI ANAFUATA (€146M)


Jana Machi 10, 2014 tovuti maarufu ya soka inayojulikana kama Goal.com, imetoa majina ya wacheza soka matajiri duniani ambapo mshambuliaji wa Ureno anayechezea timu ya Real Madrid , Christiano Ronaldo ambaye pia ni mwanasoka bora wa dunia kwa sasa, ndiye tajiri kuliko wote akiwa na utajiri wa €148million, Messi ni wa pili akiwa na €146million na watatu ni Etoo akiwa na €85million. Hii haihusishi wachezaji waliostaafu soka. Hawa ndiyo wanasoka 10 wa kwanza kwa utajiri duniani.

SEMADAT, WAWILI KWA PICHA: "SALAMA JABIR NA VANESSA MDEE"

HAPPY BIRTHDAY DIDIER DROGBA

Mcheza soka maarufu wa barani Afrika anayetokea nchini Ivory Coast, Didier Drogba ametimiza umri wa miaka 36 leo Machi 11, 2014. Mchezaji huyo ‘striker’ ambaye ndiye aliyekuwa mchezaji wa kwanza aliyezaliwa Afrika kufunga magoli 100 kwenye mashindano ya UEFA na ambaye alikuwa miongoni mwa wachezaji waliofunga magoli mengi katika historia ya timu ya Chelsea, alianza mikiki ya soka akiwa na umri wa miaka 18 aliposaini mkataba na Levallois.

Monday, March 10, 2014

MANENO YA HAMASA KUTOKA KWA ‘CEOs’ WA MAKAMPUNI MATANO (5) YA TEKNOLOJIA DUNIANI



1.Mark Zuckerberg, CEO wa Facebook

“Swali moja ambalo huwa najiuliza kila siku ni kwamba, hivi nafanya kitu muhimu sana ambacho natakiwa kuwa nafanya?. Mpaka nijihisi kama nafanya kazi kutatua tatizo flani vinginevyo siwezi kujisikia vizuri kwa jinsi ninavyoutumia muda wangu”

Sunday, March 9, 2014

CHINGY NA BOW WOW NI MIONGONI MWA MASTAA WANAOSHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA LEO


Chingy na Bow Wow ni wanamuziki  wa nchini  Marekani wanaosherehekea siku ya kuzaliwa tarehe 9 Machi.  Chingy ametimiza miaka 34 leo wakati Bow Wow ametimiza miaka 27.

Saturday, March 8, 2014

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI 2014, "USAWA NI MAENDELEO KWA WATU WOTE"


“Nchi  zenye usawa wa jinsia zina ukuaji mzuri wa uchumi, kampuni zenye viongozi wengi wa kike zinafanya vizuri,  makubaliano ya amani yanayohusisha wanawake yanadumu kwa muda mrefu, mabunge yenye wanawake wa kutosha yanakumbatia sana masuala ya kijamii ikiwa pamoja na afya, elimu,  kuondoa ubaguzi, kusaidia watoto. Imethibitika hivyo. Usawa kwa ajili  ya wanawake ni maendeleo kwa wote”.  

LUPITA NYONG’O AENDELEA KUSHINDANISHWA NA JENNIFER LAWRENCE

Kwa sasa sio tuzo za filamu bali jinsi walivyovaa, ni baada ya mtandao unaoitwa  ‘Ghafla’ wa nchini Kenya kuweka hizi picha mbili na kuuliza “Who Wore It Better?” Lupita VS Jeniffer Lawrence,

OPRAH ALIVYOWAKARIBISHA MAMA NA KAKA YAKE LUPITA KWA AJILI YA CHAKULA CHA MCHANA


Kama ilivyokuwa kwa mastaa wengi wa nchini Marekani na sehemu mbalimbali duniani kumpongeza muigizaji wa nchini Kenya Lupita Nyong’o ambaye alijinyakulia moja ya tuzo za Oscar,

RIHANNA NA LUPITA NYONG’O WAKIWA PAMOJA KWENYE ‘SHOW’ YA MIU MIU NDANI YA PARIS

Rihanna na Lupita Nyong’o walikaa pamoja mbele katika onyesho hilo la  Miu Mui  katikati ya wiki hii  jijini Paris . Picha zaidi.

CHRISTY WALTON :MWANAMKE WA KWANZA KWA UTAJIRI DUNIANI

CHRISTY WALTON wa nchini Marekani, anaungana na wanawake wengine duniani kote kuazimisha siku ya wanawake duniani akiwa ndiye tajiri wa kwanza duniani mpaka sasa mwaka 2014. Kwa mujibu wa  jarida na mtandao maarufu wa Forbes, Christy ndiye anayeongoza kwa wanawake na kwa  jinsia zote anachukua nafasi ya 9.

Thursday, March 6, 2014

ROSTAM AZIZI ATANGAZWA BILIONEA MPYA MWAFRIKA KWENYE FORBES

Rostam Azizi
Kabla ya hapo, mara ya mwisho tulimfahamu kama mmoja kati ya  matajiri wakubwa barani Afrika na tajiri wa kwanza nchini Tanzania lakini hakuwa bilionea. Sasa anabaki katika orodha hiyo lakini pia akiwa tayari ni bilionea.

Rostam Azizi amekuwa mtanzania wa kwanza kutangazwa na Jarida la Forbes kama bilionea mpya kutoka Afrika. Rostam ambaye ametangazwa kwenye orodha iliyotoka mwaka  huu 2014 ndani ya mwezi  Machi, anamiliki asilimia 35 ya hisa za kampuni ya simu ya  ‘Vodacom Tanzania’, mtandao wa simu wenye wateja zaidi ya milioni 10, pia anamiliki kampuni ya madini ‘Caspian Mining’ inayotoa huduma kwa makampuni makubwa kama  BHP Billiton and Barrick Gold. Kampuni yake ya ‘Caspian Mining’ pia inamiliki vitaru  vya uchimbaji wa madini ya Dhahabu, Shaba na Chuma nchini Tanzania.

HEBU SOMA KIDOGO HIZI 'TWEETS' ZA MPOKI 'MWARABU WA DUBAI'

NUKUU YA FARAJA NYALANDU KUTOKA KWA MAMA SALMA KIKWETE

Ikiwa ni siku mbili tu zimebaki kufikia siku ya wanawake duniani ambayo ni Machi 8, Miss Tanzania 2004 ambaye pia ni mke wa Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Lazaro Nyalandu, amemnukuu 'First Lady' wa Tanzania Mama Salma Kikwete kwa kuandika hivi kwenye akaunti yake ya Twitter:

SEMADAT, WAWILI KWA PICHA: "WEMA SEPETU NA AUNT EZEKIEL"


ALAMA 10 ZA KUKUONYESHA KWAMBA HUPENDI KUPATA MAFANIKIO



Si kweli kwamba kuna mtu ambaye hapendi kupata mafanikio,  ila ukiona alama hizi kumi kwako basi ujue unatakiwa kuwa makini.

LUPITA NYONG'O ALIVYOTUPIA INSTAGRAM BAADA KUPATA TUZO


Ni picha iliyozungumziwa sana kwenye mitandao hasa ya nchini Kenya. Lupita aliweka picha hiyo na kuandika yafuatayo: