UA-45153891-1

Thursday, March 27, 2014

BONGO QUEEN LEO NDANI YA SEMADAT


Leo tuko na mwanamuziki machachari wa kike 'Snura Mushi' ambaye ana nyimbo zenye maudhui ya pekee. Ukisikiliza wimbo wake hata kama ni mpya utajua ni yeye kutokana na mpangilio wa mashairi yake. Ni mbunifu ambaye amejitengenezea alama ya pekee kimuziki. Alianza na "Majanga", ikafuata "Nimevurugwa" na sasa ni "Ushaharibu".

Snura ambaye  pia yuko katika fani ya filamu, ameanza kutumia staili ya kuunganisha muziki wake na filamu ambapo alisikika kupitia Redio moja hapa nchini siku chache zilizopita akisema kwamba kila ujumbe wa wimbo wake utaandaliwa filamu ambayo pia itakuwa ikipewa jina la wimbo husika.

Snura ni mmoja wa wasanii waliotajwa kwenye tuzo za muziki za Kilimanjaro 2014 kwenye kipengele cha msanii bora chipukizi. 

No comments:

Post a Comment