CHRISTY WALTON wa nchini Marekani, anaungana na wanawake wengine duniani kote kuazimisha siku ya wanawake duniani akiwa ndiye tajiri wa kwanza duniani mpaka sasa mwaka 2014. Kwa mujibu wa jarida na mtandao maarufu wa Forbes, Christy ndiye anayeongoza kwa wanawake na kwa jinsia zote anachukua nafasi ya 9.
Utajiri wa Christy unatokana na kampuni ya Wal-Mart Stores, Inc ‘Walmart’ ambayo inahusika na shughuri za ‘store’. Ni kampuni ya familia ambayo ilirithiwa kutoka kwa mume wake John Walton ambaye alifariki mwaka 2005 kwa ajali ya ndege. Familia ya Christy inamiliki asilimia 50 ya hisa za kampuni hiyo. Kwa mujibu wa jarida lingine la Fortune Global 500, kampuni ya ‘Walmart’ inayomilikiwa na mama huyo, ndiyo kampuni binafsi inayoongoza kwa kuajiri watu wengi duniani.
No comments:
Post a Comment