UA-45153891-1

Friday, March 21, 2014

HUYU NDIYE MBWA ALIYENUNULIWA BEI YA JUU KULIKO WOTE DUNIANI - ZAIDI YA $1.9 MILIONI



Mbwa mwenye umri wa mwaka mmoja aina ya "Tibetan mastiff" aliyeuzwa nchini China kwa karibu dola za kimarekani milioni 2, inasemekana ndiye mbwa aliyeuzwa kwa bei kubwa kuliko wote ulimwenguni mpaka sasa kwa mujibu wa gazeti la New York Daily News. Mbwa huyo aliuzwa kwenye maonyesho ya kifahari huko Hangzhou mashariki mwa China.




 


Mwanaume ambaye hakufahamika jina lake akiwa na mbwa wawili waliouzwa kwa bei mbaya akiwemo huyo (kushoto) aliyeuzwa karibu dola za kimarekani milioni 2. Kiasi  cha bei aliyonunuliwa mbwa huyo ni zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.9.


No comments:

Post a Comment