UA-45153891-1

Tuesday, March 4, 2014

CHIMAMANDA ADICHIE AWATAKA WANAHABARI WAMUITE ‘MISS’ BADALA YA ‘MRS’


Mwandishi wa vitabu Chimamanda Ngozi Adichie anayemiliki tuzo nyingi  katika tasnia hiyo, amewaonya  waandishi wa habari nchini Nigeria waache kumuita Mrs Chimamanda Esega, ambapo inasemekana Esega ni jina la ukoo la mume wake, badala yake watumie majina yake wakianza na neno ‘Miss’ yaani Miss Chimamanda Adichie.


“Kabla sijaanza, tafadhali napenda kusema kwamba jina langu ni  Chimamanda Adichie, ndivyo ninavyotaka. Na sio ‘Mrs’ ila ‘Miss’, nasema hivi kwa sababu kuna watu utazani wamefika kanisani kupata  jina hilo, na mpaka kuniandika kama Mrs. Chimamanda (Esega). Sipendi kabisa”, Alianza kwa kuzungumza hivyo katika usaili na gazeti la TheSunNews.

No comments:

Post a Comment